Natafuta kazi

sanzy

Member
Joined
Jun 15, 2021
Posts
6
Reaction score
9
Habari za muda huu wakuu.

Naitwa Geofrey Athuman 28yr mkazi wa dar es salaam .

Natafuta kazi yoyote halali nitakayopata. Nina nidhamu, bidii, uaminifu na niko tayari kujifunza na kufanya kazi kwa juhudi.

Mwenye nafasi ya kazi au taarifa yoyote naomba anisaidie. Nitashukuru sana. Asanteni. 🙏
0763493987
 
Kila la kheri mkuu.
 
Unaweza kukimbia na mifuko miwili ya cement kichwani usiku

Duuuuuh uwezo huo ninao lakin sitakuwa nakimbiza kila siku mkuu kwakuwa mwili nao utafikia wakati utaanza kudai kupumzika na hizo kazi nimezifanya sana ety ,Sasa najarib kutafuta kazi ingine ambayo itakuwa friendl na hali yangu ya Sasa 🙏
 
Usinichafue pla, au anzisha wa kwako wewe usaidie watu!
Sasa mkuu hutaki mirejesho kwa watu waliojaribu kutafuta au kutuma CV zao kwenye moja ya nafasi ulizozipost??

Imagine mtu anatuma CV yake vizuri inapokelewa inapita muda unajibiwa eti tumia namba hii unatumiwa namba nyingine tofauti na Ile iliyopo kwenye matangazo ukienda kwenye hiyo namba tena unaulizwa kama upo kwenye group la usahili unajibu NO anakwambia lipia kiasi kadhaa tukuunge😀😀huoni Kuna upigaji mkuu wangu hapo?

Hebu kubalini na mirejesho negative ili kuzidisha weredi na kuwaokoa vijana kupigwa pesa maana sasa hivi wana mbinu ya kujihami kwa kubadilisha namba juu kwa juu ili kikiharibika watasema Wana namba moja kumbe walikuhamisha kwenye namba nyingine🚮

Yote kwa yote Mungu awasaidie tu maana kupata kazi imekuwa kazi zaidi hata ya kazi zenyewe
 
Unaweza kufanya kazi za sales?
Siku unazotoka,mtazunguka na gari ya Ofisi.
Ofa Yao 300k Kwa mwezi, Kwa kuanzia.
 
Naomba ukanitag kule post uliyoombwa pesa hapa haujasaidia ila unazidisha tu tatizo! Ulivyoombwa pesa ulitakiwa kureport na kunitag muda huo!
 
Mungu akutangulie mdogo wangu, nafaham ugumu unaopitia, ila maisha ya sasa kama unaweza Fanya umachinga ukiotea biashara Fulani katika eneo ulilopo hukosi faida ya ef 20 kwa siku, mwezi una laki SITA bila makato ya Kodi, naongea kitu amabcho nilifanya mimi mwenyewe.

Ukijiajiri unakua huru kucheki inshu zingine mfano kwa sasa naomba mungu mziki unikubari japo naona ngumu kutokana na gharama nazo kutana nazo kubwa sana ila we still move mkuu nobody knows tomorrow. Usikubali kupiganiwa kwa Kila Hali mengine pambanaa mwenyewe mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…