Samahani kama nitakua nakosea, ila naingelea kitu ambacho ndio kinafanyika humu na especially Kwenye mitandao ya jamii Kwenye swala la maombi ya kazi.
Unapopost tangazo lako la kuomba kazi, yule mtu anaetazamia kukuajiri kiukweli anaipekua sana profile lako kujua hata nusu ya mtu anaetaka kumuajiri, atasoma posts zako za nyuma, atarejea majibu yako katika post mbali mbali, ataangalia profile yako kwa makini, ndo mwisho atajudge kama huyu mtu ananistaili au lah..
Ni vyema tukawa na profile zisizo na dosari linapokuja swala la kuomba kazi humu ndio maana mkuu apo juu kakuelewesha juu ya swala la umri!!
Mfano mzuri ni Mimi.... Niliwahi kua na account nyingine, ambayo nilikuwa napost nachoona sawa, majibu kila post hata zisizomaana...afu bado naomba kazi kupitia pale pale....lakini nilijitathimini nikabadilika, nikafungua hii na kua na mipaka since nilijua tu ipo siku nitajitokeza Mbele ya umati kuomba kazi na maboss wangu wataipekua profile yangu vizuri.
Nilipokuja kupost kutafuta kazi humu,haikupita Hata week kuitwa interview, na nikapata na mpaka Leo Namshukuru Mungu. Kwaiyo tujifunze kwakweli.