Natafuta kampuni ya kununua

Changamoto2015

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2012
Posts
773
Reaction score
316
Kuna shughuli nataka kuifanya, yanipasa niwe na kampuni, kwa hivyo kama una documents za kampuni yeyote ambayo uliregister brela na kwa bahati mbaya haikufanya kazi yeyote mpaka sasa tafadhali tuwasiliane ili tuangalie taratibu za kuuziana pamoja na kubadilisha umiliki kisheria.

Tafadhali hakikisha kampuni haina scandal wala deni lolote kwa mamlaka husika (i.e. TRA, Brela or any other authority).

Kampuni ya kilimo itakuwa nzuri zaidi. Asanteni
 
Kampuni ya aina gani unataka nunua mkuu?
Mfano kama kuna kampuni ilisajiliwa ya sheria na consultancy halafu we unataka kufanya biashara lets say kwa mfano ya kuuza bidhaa kama nguo, meno ya tembo labda na kadhalika, si itakulazimu kubadilisha MEMARTS yote mkuu?
 

Kuwa specific mkuu, unataka kampuni gani; mimi ninayo ya kilimo itakufaa?
 

Na kama ni kazi umepata tu moja labda ya miezi kadhaa au ya onetime supply ningekushauri ukubaliane tu na mtu mwenye kampuni utumie kampuni yake kisha umlipe, otherwise fungua yako mkuu maana siyo kazi kivile, siku kadhaa tu utakuwa na kampuni yako, lakini kama umepata kazi kimagumashi itashangaza kazi ulipewa kabla ya usajili wa kampuni.
 
nina kampuni nilijisajili brela na nikashindwa kuchukua fomu za tin na leseni kutokana matatizo yaliyonipata kama utahitaji hivyohiyvyo nipm tufanye biashara
 

duh! yani meno ya tembo na TRA, TRA wanasajili!
 
duh! yani meno ya tembo na TRA, TRA wanasajili!

Usishangae sana mkuu. Watanzania ni wafanyabiashara wakubwa sana. Kuanzia wananchi watawaliwa mpaka viongozi wao wanaowatawala. kama meno ya tembo yanauzika, sembuse sembe?
 
Bado natafuta kampuni sijapata. Tafadhali kama uko serous ndio uweke hapa post yako. But kama hauko serious usisumbue watu wakutafute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…