Natafuta gari mpya (Hiace) ya Mkataba

Ila hizi dini, kwahiyo unadhani mtu atakukopesha gari bila kuweka riba? Au riba ina maana gani kwenu
Akikukopesha mali inakua sio riba bali ni faida, ni elimu pana kidogo ambayo ni kama hesabu za hasi na chanya.
 
Huu sio mkopo wa kufilisi mtu, huu ni mkopo kazi. Vikishindikana mwenye mali yake anaichukua na mimi naendelea kupambana na maisha mengine.
pambana kwanza na hayo maisha mengine kabla hujawaza kuwa na kitu cha mtu.
 
Ndugu yangu kitu unachoitaji ni kikubwa sana alafu tayar umemkaba muwekezaji asipate faida asa uliposema mkataba uwe wa miaka miwili.Ebu vuta picha haice mpya 5L ukiagiza japan adi inafika mkoni mwako inaweza kukulamba 32-35milion apo akuna bima,vibali vya kazi alafu wewe unataka kwa mwaka umlipe mwekezaj 18milion au 36milio kwa miaka miwili na gar iwe yako (huu ni utapeli wa kimahesabu na ukweli ata bajaj huwez pata)
 
Lizo mkristu vs Ustaadhi CoderM
 
Mko

Mkopo wa benk za kiislamu haujatimiza masharti ya mkopo wa kiislamu. Kwa sababu mkopeshaji sio mwenye kumiliki mali anayoikopesha. Kwahiyo zile ni riba zilizojificha kwenye kichaka cha faida.
Wewe hufai kupewa gari kwa haya majibu yako ya udini. Hamia Afghanistan
 
Fafanua kidogo ni wakina nani hao? Ni wauza magari au ni taasisi ya mkopo.
wao ni wakopeshaji wa magari aina zote, na mashne za viwandan na vifaa vya kilimo.
Riba lazma iwepo, maana mtaelewana mda wa kulipana
 
Vipi kama ikawa ni used tayari kwenye good condition halafu ikawa mkataba wa miaka mitatu nayo itakua utapeli? Au umeamua kuchagua upande wa kusapoti pointi yako.
 
Mwisho wa siku lazima tujue thaman ya iyo gar unayo taka kabla ujapewa mkataba wa miaka 3 maana atakaekupa mkataba nae anataka faida (maybe iyo gari iwe chini ya tsh 20milion na ukipewa mkataba wa 3yrs na ujitegemee kilakitu angalau itamlipa uyo atakaekupa
 
Vipi kama ikawa ni used tayari kwenye good condition halafu ikawa mkataba wa miaka mitatu nayo itakua utapeli? Au umeamua kuchagua upande wa kusapoti pointi yako.
I like your replies πŸ‘
 
hakuna kitu ninachokidharau sana kama huna pesa halafu unazaaa sana..
Kutokua na pesa ni kwa kipimo gani? Kwa mfano kati ya watoto watano nilionao wanne wameanza shule na hakuna hata mmoja anaesoma st. kayumba. Kwa ufupi hela ya kukidhi mahitaji ya familia inapatikana lakini kupiga hatua kadhaa mbele ndio tunazifosi.
 
wao ni wakopeshaji wa magari aina zote, na mashne za viwandan na vifaa vya kilimo.
Riba lazma iwepo, maana mtaelewana mda wa kulipana
Wakiwa wao ni wamiliki, hapo hakuna riba ila kama na wao wananunua ndio wakupe ulipe kidogo kidogo hapo ndio riba inapatikana. Asante ngoja niwafuatilie nitaleta mrejesho.
 
Umeeleza vizuri sana kama Mdomo, umenyooka
 
Kutokua na pesa ni kwa kipimo gani? Kwa mfano kati ya watoto watano nilionao wanne wameanza shule na hakuna hata mmoja anaesoma st. kayumba. Kwa ufupi hela ya kukidhi mahitaji ya familia inapatikana lakini kupiga hatua kadhaa mbele ndio tunazifosi.
Mkuu huyo jamaa achana naye, endelea na maisha yako ya kupambana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…