Mdanganywa
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 620
- 342
Eti tunalalamika kwamba watu wanapanda vyoe kwa kujikomba au kujipendekeza. KWamba msomi mzima alikuwa kipanga darasani lakini akifika kwenye taasisi au serikalini basi anaacha yale mashindano ya ukipanga anaanz amashidano ya ukilaza.
Kama ni mwandishi akiwa kilaza sana kuandika habari zinafurahisha wakubwa basi gazeti lake linapata matangazo mengi.
Kama ni ofisini, ukijipendekeza licha ya kumzidi akili huyo unayejipendekeza kwake basi utapanda vyeo, utanunua gari na kwa hakika utaishi maisha tunayosema ni mazuri.
Nasikia hata huko makanisani ili mtu uwe padri lazima huko seminari ufanye kazi ya ziaza ya kujipendekeza, tena wakati mwingine mtu akikuambiw akwamba "sema hii ni nyeupe" na wewe unasema ni nyeupe hata kama macho yako yanaona ni nyeusi.
Kwenye vyama nasikia utapatana na viongozi ukiwa ni fundi wa kujipendekeza na kujikomba.
Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kuna jambo hatufundishwi na kila mtu anajifunza kivyake.
Tnafundishwa kwamba kujipendekeza na kujikomba kwa binadamu mwenzio mwenye ubinadamu kama wewe ni kujidhalilisha. Lakini hapohapo unaona kwamba kila kona ya maisha wanaojipendekeza ndiyo wanafaidi maisha.
Ukifika kazini ukajifanya una akili nyingi kama ulivyokuwa chuoni basi sahau maisha mazuri, sahau kupanda cheo chochote. Wenzako waliongia katika mashindano ya kujipendekeza wanaondoka wakikuacha unaona.
Kama ni kwenye chama wenzako watachukua uongozi, watarithishwa uongozi na watoto wao utawaona wanasoma "nje", kwa sababu walijifanya wajinga kujipendekeza, wewe hukujipendekeza, ukaacha principle ya kufaulu kwa kujifanya mjinga, ukang'ang'ania kwamba wewe ni "genious" ukabaki hivyohivyo.
Sasa nahitimisha. Je, ni kipi chuo kinachofundisha kujipendekeza na kujikomba. Maana na mimi sasa ninataka kufaidi maisha kama wanaofaidi wanaojikomba na kijupendekeza.
Wasalaam.