Nassari Azidi kuchangiwa Arumeru

Mkuu hapa hautafutwi ubunge unatafutwa mtaji. Hivi wewe ukichangiwa shilingi milioni 100 bado unahitaji kwenda mjengoni kufanya nini?

lowasa ana ngapi?
 
Na ole wake akose ubunge halafu tukamuona anatakata kwa pesa zetu za bakuli tutamfuata huko huko FOUNDATION FOR TOMMORROW manake tunajua huko ili ale mpaka awapigie magoti wazungu.
hilo ni dua la kuku,

Mwaka huu mtaomba maombi yote issue ni mafanikio;
 

Usimwamshe aliyelala utalala wewe. Mimi nimejiamsha mwenyewe pesa yangu hamuipati tena ng'o na bakuli lenu , kumbe Ndiyo sera ya CHADEMA ya kumtoa mmoja mmoja kwa bakuli hata kama mnajua wazi kuwa ubunge hampati?. Tusidanganyane hapa kwa hili la bakuli tunawaibia wananchi jamani. Au zingine ni kwa ajili ya kulipa deni la MBOWE manake nasikia anakidai chama fedha nyingi sana. Sasa huyu naye anatugharimu ni Mwenyekiti wa Chama au ni Mfanyabiashara ndani ya Chama?
 

Ungekuwa umeamka ungekubali kutumiwa kama kondom?
 
Mkuu naona bado huelewi maana ya people's power kwa sababu hiyo pesa yako kuipata itakuwa ngumu sana ni si wewe tu mpo wengi wa aina yako. sisi tunakijenga chama tukijua kuwa ni mali yetu na haya wanayo sema viongozi wetu tunawaunga mkono si maneno tu pali kwa mali pia ili huduma isonge mbele na wsiwe na sababu ya kulala

Chadema ya leo si mali ya MBOWE zinduka wewe !!!!!
 

Hilo gamba! Unapoteza muda wako bure kumuelimisha. Hapo alipo anahaha kufanya kazi aliyotumwa na mafisadi ila hata yeye anajua kimenuka!
 
lowasa ana ngapi?

Mkuu Jog achana na huyu mpuuzi. Wamezoea kufikiria kila kitu kiccm ccm. Dhana ya wananchi wa kawaida kumiliki chama kwao halipo kabisa maana chama chao kinamilikiwa na mafisadi marafiki zao wanao miliki makapuni makubwa feki kule ughaibuni. Na mwaka huu roho zao zitawauma sana maana hakuna mwananchi atakaekubali kura zichakachuliwe ile hali wanajua waligharamikia kwa hali na mali mchakato mzima. Tazama hii short outline hapa chini:

CDM=Wananchi
CCM=Mafisadi
 
thatha

kama unajua hesabu fanya hii hapa kwenye signature yangu
 


CCM yachekesha sana. CHADEMA wakija na mbinu mpya ya kufanikisha mambo yake ccm watapoondaaa weeeee!!! Lakini mwishowa siku wakiona wameshindwa na cdm wanazidi kufanikiwa wataiiga au niseme watakula matapishi yao wenyewe.

Mfano: (1) CHADEMA walipokuwa wameanza kutumia helikopta kwenye kampeni zake za uchaguzi duuu ccm wote waliponda kweli na kwa maneno mengi ya kejeli na dharau.... nadhani kwa wanaokumbuka wanajua sana hilo. Sasa leo kiko wapi. tena wao ndo wakavunja rekodi... wakawa na helikopta zaidi ya mbili nadhani kama 3 hivi...waulize leo hii vipi mbona nanyi mwatumia helikopta!!!!!??? Kazi kuiga tuu hawana mbinu mpya

(2) Operesheni (Operation) Sangara: CDM ilipoenda mikoani ccm wakaja nyuma yao eti kuweka mabo sawa....kujibu mapigo

(3) Kuchangiwa na wananchi kwenye hii mikutano ya Arumeru mashariki..... CCM watakuja iga....????

(4) n.k.....mengine weka wewe....

Na naamini CCM wakiona CHADEMA kinafanikiwa kwa njia hii ya kuchangiwa na wananchi ktk mikutano yao...usishangae hii nayo watakuja iga pamoja na maneno yote ya kejeli wanayotoa leo... Hata maandamano ccm wangekuwa wanaweza kupata watu kwa hiari yao kuja kwenye maandamano nayo hiyo wangeiga, tatizo ni tu watu hawaitikii kwa hiari yao kwenda ccm mikutanoni, kuna gharama kubwa ya kuwaita..kuwabeba... toka mbali....

Mimi nimefuatilia sana sasa, ni kama vile ccm haina kitu/mbinu mpya katika kuwashawishi wananchi..wanangoja kujibu mapigo kama vile wao ndo chama cha upinzania sasa na cdm ndo chama tawala.

Angalia hata uzinduzi wa kampeni nyingi cdm ndo wataanza, kisha ccm watafuata na mkutano mzima ni kujibu mapigo ya hotuba za cdm na kutoa kejeli kwa cdm...sasa ni kama vile ccm wamepoteza kujiamini...

Naishauri ccm ikae chini ije na mbinu zao mpya iache kungojea cdm watafanya nini na waje kujibu mapigo au kufuata nyuma ya cdm kwenda kuweka mambo sawa
 
Mkuu hapa hautafutwi ubunge unatafutwa mtaji. Hivi wewe ukichangiwa shilingi milioni 100 bado unahitaji kwenda mjengoni kufanya nini? pamoja na ujinga wote unaoandikwa tutamchangia tu mdogo wetu Nasari mimi nimechanga sh 16,000
 

vipi hapo na kupiga kura mtakodi watu au?
 
Pesa za ruzuku wale MBOWE na SLAA halafu wakati wa uchaguzi utembeze bakuli! hii imekaaje siyo kuwaibia wananchi?
Dalili za kukubalika kwa chama cha kisiasa ni uungwaji mkono kwa vitendo na watu walio wengi. Kuchangisha michango katika uchaguzi ni njia ya kufaa inayotumiwa na vyama vyote vya kidemokrasia duniani ili kupima uungwaji mkono. Mfano, Democrats ya Obama, iliipita Republican kwa michango toka kwa wamarekani 2008. Vyama hivyo vyote ni tajiri na viko katika nchi tajiri zaidi duniani. Mbona kila uchaguzi vinapitisha bakuli? Ila kwa Tanzania, CCM hali ni tofauti, ni kwamba hakiungwi mkono na watu wengi ndio sababu hata wakiomba michango wanaotoa ni matajiri tu (Rejea uchaguzi 2010). Ili iungwe mkono CCM imekuwa ikitoa michango (Rushwa?) kwa watu, badala ya kupokea michango toka kwa watu.
 
Pesa za ruzuku wale MBOWE na SLAA halafu wakati wa uchaguzi utembeze bakuli! hii imekaaje siyo kuwaibia wananchi?

wanaochangia wengi wao ni wana Arumeru kwa mtu wanayejua atawaletea maendeleo.
huenda huna cha kuchangia au umezoea kupewa khanga na kofia kukopu na hii staili huwezi!
 
wananchi wameonyesha kuwa WAPO PAMOJA NAYE ...........CHANDA CHEMA HUVIKWA PETE

sidhani kama aliomba mchango .......wenyewe kwa KUMPENDA MBUNGE WAO MTARAJIWA:violin::violin:
 
slogani ya CDM ni peoples power hivyo wananchi wanajukumu la kushiriki kwa kila hatua kufikia lengo kwa kutumia rasilimali walizonazo.

Songa mbele JN hope utafika mjengoni kutetea wana Arumeru achana na Wana JF Maslahi.
 
Chadema ni chama cha wananchi. Let's them contribute for it.
 
wanaochangia wengi wao ni wana Arumeru kwa mtu wanayejua atawaletea maendeleo.
huenda huna cha kuchangia au umezoea kupewa khanga na kofia kukopu na hii staili huwezi!

Jibu hoja pesa ya ruzuku inatumika wapi? Au ndiyo kumlipa mshahara Padre Slaa na maposho kwa wabunge wote mliowaleta huku Arumeru mashariki manake ndiyo kawaida yenu kupeleka wabunge wenu wote mjimboni kama mlivyofanya Igunga na Uzini na ikala kwenu,alafu pesa zingine mnamlipa Ndesambulo huwa anawakodisha headkopta yake kwenye kampeni zenu na pesa zingine viongozi wa chama chenu chadema wanakiuzia chama magari used kwa bei kubwa bila huruma,chama kinakuwa hakina pesa inabidi mchangishe watu huo ni utapeli wa mchana watanzania wamewajua na hawawachaguhi mtaona kitakachowapata ni zaidi ya igunga na Uzini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…