Awali ya yote amani iwe kwenu wana jamvi.
Katika siku za hivi karibuni, nimekuwa nikizungukia maeneo mengi, lakini kitu kinachokuwa kinanipa shida ni kuwa, kokote ninakopita, nyuso za watanzania wenzangu 'zimepoteza' furaha kabisa, sio nyuso za watanzania wale wa kipindi cha nyuma, nyuso zilizokuwa zimejaa bashasha, tabasamu na furaha nyingi, ucheshi sasa haupo miongoni mwa watanzania, ukimpiga kikumbo kidogo tuu kwa bahati mbaya, matusi utakayoambulia hapo utajuta.
Sasa najiuliza, hii yote inasababishwa na nini? Mbona ule upendo na amani vilivyokuwepo miongoni mwa watanzania vinayeyuka kwa kasi mithili ya theruji iliyokumbwa na jua kali? Tatizo hasa ni nini?
Wanajamvi, hebu tusaidiane kujua nini hasa chanzo, na nini kifanyike.
Karibuni.