Nashindwa kumuelewa mke wangu kuhusu kupima VVU

chanawaleti

Senior Member
Jul 4, 2016
176
209
Naumia kwa kuwa mke wangu ni mjamzito miezi mitatu now, nimejaribu juzi kumwomba kwenda clinic ananiambia Muda bado, mimi nilishamueleza kuwa tayari nilipima na nikawa tayari nina maambukizi, yeye anasali Sloam church tenda neno shika neno.

Sasa yeye kwa imani yake anasema kupima hapimi kwa kuwa anauhakika hana kwa imani yake sasa nilimbembeleza wiki iliyopita tukiwa wote kakataa, nimerudi nilipo jana nikamgusia aende clinic acha aniwashie moto hataki kusia na mpaka leo simu yangu hapokei kabisa.

Mimi lengo langu ni twende clinic mapema ili kama kaathirika tujue njia ya kumkinga mtoto na maambukizi ili azaliwe salama sasa yeye hataki naumia moyo maana anasema ataenda kwa Muda wake sasa sijui ni lini sasa najiuliza akienda na miezi sita si atakua mtoto kuambukizwa? "Je nitumie njia gani aelewe maana nimejishusha kwa cares but hanielewi kabisa.
 
Pole kwa mtihani mzito ndugu.
Kwa mbaali naona mbinu za kidiplomasia hapo kama zinaanza kufeli..
Mi nakushaur kama diplomacy imebuma hebu tafuta rafiki/ndugu yenu wa karibu ambae mnaminiana ajaribu kumuelezea.. Kingine ni kwamba lazima umuweke wazi juu ya maambukiz kwenda kwa mtoto.. Akikaza na hapo jaribu kuwashirikisha wazazi wenu.. Akikataa na hapo tumia UDIKTETA, hat ukiwa uchwara haina shida ,tumia force king mpaka akapime..
Simply ni kwamba vita inakuja baada ya diplomacy kushindikana, akizingua tumia ubabe ndugu...
Hayo ndo makanisa yetu ya ufufuo.. Dada angu alijifanya anaacha dawa kisa kaambiwa kanisani kua kapona.. Daaadek hao wala cd4 walivoanza kushambulia kasi mbona alirud hosptal..
 
.. Akikataa na hapo tumia UDIKTETA,
Hakuna haja ya udikteta, kwa Sasa mwanamke mjamzito kupima ni lazima siyo hiyari, akianza cliniki tu ni lazima apime, na mtoto anaambukizwa VVU wakati wa kuzaliwa, akiwa tumboni yuko safe kabisa, ngoja waje wataalamu wa afya wamshauri vizuri, but hapa asiumize kichwa. Ni vizuri yeye ameshajitambua ataishi kwa tahadhari asiambukize wengine.
 
Nakubali mdau.. Thnx kwa marekebisho..
 
Hakuna haja ya udikteta, kwa Sasa mwanamke mjamzito kupima ni lazima siyo hiyari, akianza cliniki tu ni lazima apime, na mtoto anaambukizwa VVU wakati wa kuzaliwa, akiwa tumboni yuko safe kabisa, ngoja waje wataalamu wa afya wamshauri vizuri, but hapa asiumize kichwa. Ni vizuri yeye ameshajitambua ataishi kwa tahadhari asiambukize wengine.
asante mkuu
 
Pole sana Mkuu, huyo lazima alikuwa anajua amewaka na usishangae kukuta anatumia ARVs siku nyingi sema kadi ya CTC anaiweka kwa mama yake au rafiki yake.

Usicheze na wanawake mkuu especially hao wa hayo makanisa
 
mhhhhhhh
 
Nadhan hili bango lazima litamkamata mkeo
1468357466418.jpg
 
Muda ukifika tu atapima.ila haya makanisa na imani zao yataharibu future za watu.
 
Tatizo sio yeye.tatizo huko kanisani.sijui huwa wanaambiwaga kwa mbinu gani.wanakuwa hawasikii .wanaamini waliyoambiwa kanisani tu.kuna mmoja aliambiwa yeye hatopata maambukizi na mwenza wake.akaacha kutumia condom nae maana aliamini. Matokeo take na. yeye akaja akapata.alikuja juta.karibu kumtishia kuwa unaniulia mwanangu makusudi na sitokusamehe kwa hilo.mwambie ajaribu kutumia akili kwani ni faida yenu wote.mwambie nitalishitaki Hilo kanisa kwa kupotosha.maybe baadae ataamka
 
Pia Niliwahi Sikia Kwamba Kuna Kanisa Waumini Wake Kuongezewa Damu Ni Zambi. Vipi Mkuu Mkeo Nae Ni Kati Ya Watu Wanao Amini Hivyo?.
 
pole sana bro,kwakweli haya makanisa nikama vile yamejaa mapepo..angalau angekua anasali kwa mzee wa Upako yule ni muwazi sana na angekwambia ukweli....mlazimishe aende hosptali au panga nesi aje hom ampime kwa nguvu
 
Kwani huwa clinic inaanza mwezi wa ngapi wa ujauzito???
Inategemeana, kama ujauzito hauna complication zozote hata miezi mitano.Ingawaje kitaalamu wanashauri mara tu ugunduapo ni mjamzito anza clinic.
 
Tatizo sio yeye.tatizo huko kanisani.sijui huwa wanaambiwaga kwa mbinu gani.wanakuwa hawasikii .wanaamini waliyoambiwa kanisani tu.kuna mmoja aliambiwa yeye hatopata maambukizi na mwenza wake.akaacha kutumia condom nae maana aliamini. Matokeo take na. yeye akaja akapata.alikuja juta.karibu kumtishia kuwa unaniulia mwanangu makusudi na sitokusamehe kwa hilo.mwambie ajaribu kutumia akili kwani ni faida yenu wote.mwambie nitalishitaki Hilo kanisa kwa kupotosha.maybe baadae ataamka
Hapana bibie,hakuna tiba KAMA DAMU YA BWANA YESU,hata ukimwi ukiwa vipi,ukiombewa baaaasi ukimwi kwishney.
 
Back
Top Bottom