Nashindwa kumuelewa huyu aliyekuwa shemeji yangu

Itakua alikutana na mkaka aliemfundisha dunia ilivyo... Sasa anajutia maamuzi yake
 
hayakuhusu kabisa waache na mapenzi yao angalia mapenzi yako
 
Nina kaka yangu ambaye alikuwa kwenye mahusiano na binti mmoja waliyekuwa wakisoma wote chuoni. Uhusiano wao umedumu kwa miezi 15. Katika mahusiano yao wamekuwa na mikwaruzano ya hapa na pale.ambayo ni jambo la kawaida katika mahusiano.

Kwa sasa kaka anaishi Arusha na binti yupo Moshi, ilipofika week moja kabla ya pasaka mahusiano yao yaliingia tena mushkeri ambapo siku ya alhamisi kuu , binti alimtakia kaka , anahisi kwa sasa upendo aliokuwa nao kwa kaka yangu umeisha , hivyo kuna kijana mwingine anayefanya naye kazi, anahisi anampenda.

Baada ya kutoa ya moyoni kaka alikubal alichoambiwa. Na uamuzi aliochukua ni kukata mawasiliano ya yule binti , na akaamua kuendelea na pilika zake za kila siku za kumuingizia kipato. Baada ya kupita week moja yule binti akaanza kumtafuta kaka , anadai ana misi kuwasiliana nae, so wawe wanawasiliana kama marafiki wa kawaida, siku ya pili yule binti akamuomba kaka afike mahal anapoishi huko Moshi kwan nafsi yake inakosa amani kutokana na ukimya wa kaka yangu.

Sasa nashindwa kumuelewa huyu shem , maana kuna siku aliwahi kumwambia kaka kabla hawajaachana kwamba hajisikii kabisa kuwasiliana nae. Na anamuoa brother kama stranger ndio maana walipoachana kaka aliamua kukatisha kabisa mawasiliano.
 

Attachments

  • FB_IMG_1491796919892.jpg
    FB_IMG_1491796919892.jpg
    40.7 KB · Views: 21
Back
Top Bottom