Habari za majukumu wadau wote wa JF.
Binafsi ninashangazwa sana na kauli zinazoendelea kutolewa na wabunge wa CCM eti wabunge wa upinzani hawana uzalendo na wanatetea wezi wa rasilimali za taifa letu hususani madini. Kiukweli hivi ni vichekesho.
Hivi ni kweli wabunge wa CCM wanastahili kujivisha uzalendo dhidi ya taifa hili? Si hawa hawa walioshangilia mikataba ya madini kusainiwa nje ya nchi tena kwa mrahaba wa 3%?
Si wabunge hawa hawa wa CCM waliopitisha kwa hati ya dharula sheria ya madini yenye Kila aina ya wizi na unyonyaji?
Siyo hawa hawa viongozi wa CCM na wabunge wake wanaoendelea kuficha mikataba ya madini kwa lengo la kuficha uovu uliomo katika mikataba hiyo?
Ni nani walikuwa wanatetea wizi katika makampuni ya IPTL na ESCROW? Nani walisaini mikataba hiyo? Ni wapinzani?
Au kwa wabunge wa CCM huo ndio uzalendo?
Juzi wakati waziri wa fedha alipokuwa anawasilisha bajeti ya serikali wabunge hawa walikuwa wanashangilia na kupiga meza mwanzo mwisho na kusifia kuwa ile ni bajeti ya wananchi na imejali watu wa chini kabisa. Lakini ukiiangalia bajeti hii kwa jicho la umakini utagundua kuwa imepunguza mzigo kwa matajiri na kuwaongezea wananchi maskini kabisa wa kijijini.
Serikali imeondoa kodi toka kwa matajiri na kuwalundikia masikini halafu wanashangilia. Nonsense!
Ni hawa hawa wanaminya demokrasia ndani na nje ya bunge halafu wanajiita wazalendo.
Hakika nawachukia sana wabunge wa CCM kwa kuwa ndiyo chanzo cha nchi yetu kuwa hapa ilipo leo.