Akiwa anahutubia wananchi huko Njombe katika viwanja vya polisi vya Makambako amesema kuwa ana imani na tume ya katiba kuwa italeta katiba nzuri na hivyo wale wote ambao wanapingana na tume ni wale ambao mambo yao hayajawekwa hivyo ni wa kupuuzwa .
Aliendelea kusema kuwa Chadema hawajui hata katiba yao na hivyo hawataweza kuijua katiba ya nchi , katika kujenga hoja yake hiyo kasema kuwa mfumo wa kanda ambazo zinazinduliwa na Chadema hazipo kwenye katiba ya chadema ya mwaka 2006 na hivyo hata kama wakikabidhiwa nchi hawataheshimu katiba ya nchi .
Nnape , kwa kuwa unashauriwa na Mtela na Shonza , soma katiba ya Chadema kuhusu Kanda , inapatikana ibara ya 7.6 ,inasomeka ifuatavyo, 'patakuwa na majimbo ya chama kwa taratibu zitakazowekwa na Baraza kuu,kutokana na mahitaji ya kisiasa,kiuchumi na kijamii'
Ibara ya 7.6.1 inasema kuhusu wajumbe wa baraza la uongozi
ibara ya 7.6.2, inazungumzia kazi za baraza la kanda /jimbo
7.6.3. Inazungumzia vikao vya baraza la uongozi .
aidha, kanuni za chama zimefafanua zaidi na kwa ufasaha , hivyo kama unaweza kusema kuwa kanda za Chadema sio suala la kikatiba basi utakuwa mbumbumbu wa katiba ya chadema kupindukia na hivyo inawezekana hata ukawa mbumbumbu wa katiba ya nchi kwani kama unashindwa kusoma na kuielewa ya Chadema ,je! Ya nchi umewahi kuielewa?
Nimeishia hapo darasa la leo.