Nape: Tutazuia mafuriko kwa kidole

Nape: Tutazuia mafuriko kwa kidole

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama hicho kina uwezo wa kuzuia mafuriko hata kwa kidole, achilia mbali mikono.

Nape ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Mtama mkoani Lindi, alisema hayo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Nyangao na kuhudhuriwa na mgombea mwenza -wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano huo, Nape aliwabeza wanachama waliowania nafasi ya urais kupitia CCM na ubunge, kisha wakatemwa na baadae wakaamua kuhama.

"Mimi sizuii mafuriko kwa mkono, uwezo wangu ni kuzuia mafuriko hata kwa kidole," alisema Nape.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, jimbo lake litaongoza kwa kutoa kura nyingi za urais."Ni aibu jimbo analotoka katibu mwenezi taifa, lishindwe kutoa kura za kutosha za urais," alisema.

hatua nyingine, aliitaka Serikali kukirejesha mikononi kiwanda cha kubangua korosho kilichopo ili kiwape ajira vijana wengi ambao hawana ajira jimboni humo.

"Wanatunyonya, wakati mwalimu anaondoka kusini kulikuwa na viwanda vya korosho wakaviua, tunaomba turudishiwe kiwanda chetu cha kubangua korosho vijana wetu hawana kazi," alisema.

Nape alilalamikia tatizo la maji linalowakabili wananchi wa jimbo hilo na kusema waliowaagusha ni Benki ya Dunia ambayo imeshindwa kutoka fedha za maendeleo kwa wakati.

Akijibu hoja hiyo, Samia alisema mfumo wa stakabadhi ghalani ulianzishwa kwa nia njema na Serikali, lakini watendaji wa vyama vya ushirika waliukoroga.

"Tunataka mkulima wa korosho alipwe fedha zake anapopeleka mazao sokoni na si bonsai…Serikali ya awamu ya tano itaongeza thamani ya bei ya korosho na ufuta, tutajenga viwanda vya ushirika mtakaounda wenyewe ili mpaki vizuri bidhaa zenu," alisisitiza Samia.

Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani alisema Serikali itahakikisha inakarabati mfumo huo na kusisita haitowavumilia watendaji wa vyama vya ushirika wazembe.

Akijibu ombi la Mtama kuwa wilaya, Samia aliwaomba viongozi kufuata utaratibu wa kisheria na kuahidi kulisimamia jambo hilo.
.
Chanzo: Mtanzania
 
Duh...this is too low!
..Nani wameviua viwanda?
..Alifikiri vizuri kabla ya kuisingizia benki ya dunia kuwa imesababisha tatizo la maji!?
 
Wizi mtupu. Mbona wanaongea kama wapinzani? Kwani si serikali yao ambayo ilikuwa madarakani?
 
Duh...this is too low!
..Nani wameviua viwanda?
..Alifikiri vizuri kabla ya kuisingizia benki ya dunia kuwa imesababisha tatizo la maji!?

Hilo nalo neno!! Hivi kuna project ambayo haitegemei msaada hapa Tanzania??
 
Wizi mtupu. Mbona wanaongea kama wapinzani? Kwani si serikali yao ambayo ilikuwa madarakani?

Mind you huyo ni Katibu Mwenezi na anaongea namna hyo.....eti wanatunyonya.....akina nan??
 
Nape unatukera wenzio, unakuwa ka mpinzani sasa wananchi wa mtama tuamuaje sasa?
 
Nape mungu atakulinda umesimamiya chama cha mapinduzi kama baba yako mzee mnawiye alikuwa muadilifu sana kwenye chama
 
Nape mungu atakulinda umesimamiya chama cha mapinduzi kama baba yako mzee mnawiye alikuwa muadilifu sana kwenye chama

Kuna prof na Musa...ambaye nilicheza naye sana Dansi...Ila hana akili mbovu kama ya huyu dogo ya kutumwa tumwa na kupayuka.
 
Duh, hizi ndoto za mchana ni mbaya sana!!
Sijui ni lini Nape atazinduka kwenye huo usingizi wa pono!!
 
Back
Top Bottom