Nape, thamani yako ndani ya CCM iko wapi ikiwa aliekutishia bastola mpaka leo hii hajakamatwa?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,706
149,942
Hii ni habari katika gazeti la TanzaniaDaima la siku ya leo.

Sasa ndugu yangu Nape hebu jiulize thamani yako ndani ya chama chako iko wapi ikiwa mtu alietenda kosa la kukutishia uhai wako kwa bastola tena hadharani bado anadunda uraiani?

Siimanishi uhame CCM bali unapaswa kutafakari kauli yako kuwa CCM ni chama bora na hili liwe funzo kwa wengine wote mnaomini mmekipigania chama.

Nimejiuliza swali hili nikikumbuka maneno ya Yesu aliyoyatamka wakati anateswa na Wayahudi akiwa njiani kwenda kusulubiwa msalabani ambapo aliuliza swali hili:

"Ikiwa mti mbichi mnautendea hivi,je itakuwaje kwa mti mkavu?"

Maneno haya ya Yesu Kristo yalinigusa sana na kamwe hayawezi kutoka kichwani mwangu na ndio maana nimewaza hivi kwa ndugu yetu Nape.
 
Mkuu Kwa upande wangu Nape namuelewa sana,

Mwache akae kimya na aendelee kusifia wakati huu, anaepusha mengi

Hivi akimtaja aliyemshooshea bastola itakuwaje? Yeye anamjua vizuri, tumwache kijana wa watu, alipanda kunde kavuna jugu
 
Nakumbuka wakati ccm walipoanzisha kilichokuwa kinaitwa kujivua gamba . Nape aliulizwa mbona kama watu wanaofikiriwa kuwa gamba ndani ya ccm ni watu wazito sana? Kwa kujiamini Nape alijibu samaki anakuwa na nguvu akiwa ndani ya maji tu. Ukimtoa ndani ya maji hana nguvu yeyote. Japo mwisho wa siku hawakuthubutu kumvua yeyote gamba kwani kwa hakika ccm ingetikisika. Juzi tumeshuhudia Nape anatumbuliwa asubuhi na mchana anatishiwa kwa bastola na kwa kuwa alishatoka ndani ya maji hakuweza kufanya chochote. Maneno yake yalimrudi yeye mwenyewe.
 
Hii ni habari katika gazeti la TanzaniaDaima la siku ya leo.

Sasa ndugu yangu Nape hebu jiulize thamani yako ndani ya chama chako iko wapi ikiwa mtu alietenda kosa la kukutishia uhai wako kwa bastola tena hadharani bado anadunda uraiani?

Siimanishi uhame CCM bali unapaswa kutafakari kauli yako kuwa CCM ni chama bora na hili liwe funzo kwa wengine wote mnaomini mmekipigania chama.

Nimejiuliza swali hili nikikumbuka maneno ya Yesu aliyoyatamka wakati anateswa na Wayahudi akiwa njiani kwenda kusulubiwa msalabani ambapo aliuliza swali hili:

"Ikiwa mti mbichi mnautendea hivi,je itakuwaje kwa mti mkavu?"
Acha ushambenga ! Mambo ya bastola yameshapita !
 
Siasa ni mchezo mchafu sana. Wanasema hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu. Usithubutu kumwamini hata yule unaedhani anaaminika.
 
Hii ni habari katika gazeti la TanzaniaDaima la siku ya leo.

Sasa ndugu yangu Nape hebu jiulize thamani yako ndani ya chama chako iko wapi ikiwa mtu alietenda kosa la kukutishia uhai wako kwa bastola tena hadharani bado anadunda uraiani?

Siimanishi uhame CCM bali unapaswa kutafakari kauli yako kuwa CCM ni chama bora na hili liwe funzo kwa wengine wote mnaomini mmekipigania chama.

Nimejiuliza swali hili nikikumbuka maneno ya Yesu aliyoyatamka wakati anateswa na Wayahudi akiwa njiani kwenda kusulubiwa msalabani ambapo aliuliza swali hili:

"Ikiwa mti mbichi mnautendea hivi,je itakuwaje kwa mti mkavu?"

Maneno haya ya Yesu Kristo yalinigusa sana na kamwe hayawezi kutoka kichwani mwangu na ndio maana nimewaza hivi kwa ndugu yetu Nape.
Katika watu wenye fikra za chini sana wewe ni nambari one
 
Ni yule aliezunguka nchi nzima na Kinana kupigania uhai wa chama na ni yule alieshiriki kikamilifu kwenye kampeni za chama mwaka juzi kuhakikisha CCM inabaki madarakani.
Yeap! Ukishafanya mambo ya hovyo hovyo kiasi hicho, unawezaje kutegemea upewe kazi kubwa ya Uwaziri?
 
Ni yule aliezunguka nchi nzima na Kinana kupigania uhai wa chama na ni yule alieshiriki kikamilifu kwenye kampeni za chama mwaka juzi kuhakikisha CCM inabaki madarakani.
Naona ni yule aliyetoa siri ya goli la mkono ...!!
 
Back
Top Bottom