Nape safi ila chama anachokitumikia

Nape safi ila chama anachokitumikia

davidmgombele

Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
29
Reaction score
2
nape ni kijana focused na integrity yake iko juu lakini namuonea huruma anapojaribu kutetea chama chake cha ccm juu ya tuhuma mbalimbali zinazotolewa kwa chama chake. Namuonea huruma kwa sasa hawezi kuongelea vita juu ufisadi, namuonea huruma kwa kuwa Edward Lowassa sasa anakuja juu na anajijenga, rejea chaguzi za ndani ya chama mwaka jana, watu wake wengi wamepeta. Lazima ujue Nape sijui atatokea mlango gani maana yeye na Lowassa wameanza tag of war miaka mingi tangu enzi za jengo la vijana alipomrudhia kombora Lowassa kuwa anahusika na mkataba wa kifisadi na jengo hilo kilichompata Nape anakikumbuka. Namhurumia kwa kuwa dini ya 'CCM' anayoitumikia sio ile anayoiamini ndani ya moyo wake. Maskini msimamo wake sio ule wa chama chake. anachokisema sio anachomaanisha. Haya yote anayafanya kwa ajili ya mkate tu. Kundi lao la makamanda wa ufisadi sasa hawawezi kujitambulisha maana wameshapoteza identity.

Ushauri kwake: Ukishindwa kupingana nao ungana nao- ndicho alichokifanya aliekuwa kamanda wa vita dhidi ya ufisadi.

pole sana ndugu unayeitwa jembe la CCM
 
Back
Top Bottom