Nape Nnauye ameanza kukomaa kisiasa

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,904
7,817
Sifahamu anayemkochi, lakini Nape amekuwa mweledi kisiasa na atafika mbali.

Soma kauli zake:
"Si jambo zuri upinzani ukakosa kuungwa mkono, ni vizuri wakajiimarisha na kutoa upinzani zaidi kwa chama tawala" hiyo ni baada ya matokeo Serikali za Mitaa.

''Natoa salamu za mwaka mpya kwa watanzania wote, wana CCM na majirani zetu wa upinzan'' salaam za kufunga mwaka za waheshimiwa.

''Sintokuwa kiranja balli mlezi wa ninaowaongoza''. Baada ya kuteliwa waziri. Akaongeza: "Sheria zinapaswa kuturahisishia na si kutukwaza, tutairudisha bungeni kwa mabadiliko.''

"Ni muhimu ia kukosoa, kushauri na sio kupongeza hotuba ya rais, Nitamfikishia Rais maoni yenu''. Mkutano TAHLISO ulìofanyika Nkrumah hall.

Bila siasa safi hatufiki popote. Simbachamwene iga, Mwigulu, Bulembo, Musukuma, Jenesta nk.
 
Last edited by a moderator:
Nape na January wamesha zijua siasa za Tanzania, wanachanga karata zao vizuri. Tanzania ukitaka kufanikiwa uwe ndumila kuwili unauma na kupuliza, pia uwe kama Marekani usiwe NA rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu utakula bata.

Pia ujioneshe uko tayari kufia chama kama jamaa alivyo piga MTU makofi akawa DC.

Naomba niishie hapa nisije shikwa KWA kukiuja Cyber crime alie lala usimuamshe.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom