Mkuu Nape heshima Mbele! Kwanza ningependa vijana wenzangu tuwe na staha tunapojadiliana na viongozi wa kitaifa humu.kama huna hoja usiandike chochote tu tena yasiyo na staha.pili hiyo makala mwandishi amebeba kila kitu kutoka humu kwenye thread aliyoanzisha Mchambuzi ambaye hata yeye amekiri takwimu za asilimia 40 na 60 alikisia tu.nategemea Mchambuzi atakuja kusimamia hoja zake kwakuwa umejitokeza.mwisho nakuunga mkono vita ya ufisadi na umejaribu(Lakini inajulikana wazi kuwa CC ilijiuzulu ili kumpisha mwenyekiti aiunde upya, baada ya lawama kwamba haikuwajibika vema kuleta ushindi wa kishindo mwaka 2010. Ilitokana pia na lawama za wanachama na baadhi ya viongozi dhidi ya katibu mkuu aliyekuwapo, Yusuph Makamba na sekretarieti yake.)
Inajulikana na nani???????
Pia mkuu kwenye vita ya ufisadi tuweke itikadi pembeni ungana na Chadema kama hatua ya kizalendo kuikomboa nchi yetu.CCM imeoza na inaweza kukugharimu kwa kujaribu kwako.kubali mkuu hali ni mbaya na makundi yamejaa
Naomba samahani jana nilibanwa na maandalizi ya MIAKA 35 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi nikakosa muda wa kuja kujibu hizi shutuma usiku. Mnisamehe sana mliosubiri.
(Kwanza, alikiri kwamba vita ya ufisadi nchini illibuliwa na CHADEMA. Kwa mantiki hiyo, CCM haiwezi kujidai kwa kupiga vita ufisadi, kwa sababu jukumu kubwa ililo nalo ni kujitetea dhidi ya tuhuma za ufisadi ndani yake.)
..... Pengine tumepotoshwa sana katika vita hii ya ufisadi. Tukiwa wa kweli vita hii ilianza rasimi nchini wakati wa Azimio la Arusha na kusimamiwa sana na Marehemu Sokoine, ambao wote Sokoine na Azimio la Arusha ni kazi nzuri ya TANU na baadae CCM. KWA HOJA hii pekeake ukiacha zingine nyingi si kweli kwamba vita hii ya ufiasdi ilianzishwa na Chadema nchini, ilianza toka enzi za WAHUJUMU UCHUMI. kwa kuyajua haya SIWEZI KUSEMA KAMA MTOA HOJA ANAVYODAI, ETI NIMEKIRI KWAMBA VITA HII ILIANZISHWA NA CDM.
Hapana mkuu sijamaanisha uje Chadema bali ufisadi usipiganwe kiccm au kichadema bali kwa sura ya maslahi ya taifa.mfano tunaposema Chenge ashtakiwe kwaajili ya issue ya radar hata wewe unapaswa kusema wazi kuwa kweli wafikishwe mahakamani(hayo ya kuvuana uanachama si sehemu ya uwajibikaji kisheria!).nakusifu kwa kujaribu kusema waliyoshindwa hata wazee wa chama lakini wanapaswa kuona hutanii kwa jinsi utavyojenga hoja na kushauri serikali ichukue hatua kali na haraka! Ushahidi uph unahitajika ktk issue za Richmond,EPA? Kuwa wazi kwa dhati kuwa sheria ichukue mkondo otherwise waachie chama njoo mtaani una masters wewe!Nakubaliana na wewe kuweka itikadi pembeni kwani ufisadi hauna itikadi, lakini unaposema hivyo na wakati huohuo unaniamnia niahamie cdm maana yake umetolea itikadi kwa mkono mmoja na kuurudisha kwa mkono wa pili.h
(Kwanza, alikiri kwamba vita ya ufisadi nchini illibuliwa na CHADEMA. Kwa mantiki hiyo, CCM haiwezi kujidai kwa kupiga vita ufisadi, kwa sababu jukumu kubwa ililo nalo ni kujitetea dhidi ya tuhuma za ufisadi ndani yake.)
..... Pengine tumepotoshwa sana katika vita hii ya ufisadi. Tukiwa wa kweli vita hii ilianza rasimi nchini wakati wa Azimio la Arusha na kusimamiwa sana na Marehemu Sokoine, ambao wote Sokoine na Azimio la Arusha ni kazi nzuri ya TANU na baadae CCM. KWA HOJA hii pekeake ukiacha zingine nyingi si kweli kwamba vita hii ya ufiasdi ilianzishwa na Chadema nchini, ilianza toka enzi za WAHUJUMU UCHUMI. kwa kuyajua haya SIWEZI KUSEMA KAMA MTOA HOJA ANAVYODAI, ETI NIMEKIRI KWAMBA VITA HII ILIANZISHWA NA CDM.
Baba yenu mpya wa taifa CCM ananuka ufisadi