Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Binafsi nimekuwa nikiwafuatilia wanasiasa wetu hapa nyumbani Tanzania na Afrika kwa ujumla, kwa kweli wengi wao nashindwa kuwaelewa wanasimamia nini hasa
Moja ya changamoto kubwa tuliyonayo barani Afrika ni kuwa na wanasiasa wengi, wenye kuendesha siasa za madaraka kuliko siasa za kuwaletea maendeleo watu wao wanao waongoza, tatizo lingine kubwa na lenye kuleta utata mkubwa, ni kushindwa kutenganisha mwanasiasa na mwanaharakati
Binafsi nawaheshimu zaidi mwanaharakati kuliko mwanasiasa, sababu kubwa ni kuwa, wanaharakati walio wengi usimamia haki za wanyonge zaidi na kupigania maendeleo ya nyaja zote katika jamii zao, kuliko wanasiasa ambao wengi wao utazama maslahi yao zaidi na watu wao wa karibu
Baada ya utangulizi huo, tumtizame mh Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu, binafsi namtizama mh huyu kwa nafasi mbili tofauti, moja kama mwanaharakati, mbili kama mwanasiasa
Kwa upande wa mwanaharakati, namheshimu sana tena sana mh Tundu Lissu, ni ukweli usiopingika kwenye miaka ya 90 mwishoni, wakati huo nchi yetu ikianza harakati za uchimbaji wa madini, moja ya watanzania wachache walio simama kidete, kuakikisha nchi yetu inatunga sheria zitakazo tunufahisha na rasilimali hizi, ni mh Tundu Lissu, mpaka kuna wakati aliwahi kuwa na kesi ya uchochezi kutokana na harakati zake hizo, kwa hilo nitamuheshimu sana, alipigania kwa dhati maslahi ya nchi yake, kwa bahati mbaya hakufanikiwa sheria ikapitishwa na uchimbaji kuanza, hiyo yote ni kwa sababu alikosa support kutoka kwa mamlaka husika na sisi wananchi wote kwa ujumla wetu
Sasa ukimtizama mh Tundu Lissu kama mwanasiasa hapo ndipo nashindwa kumuelewa kabisa, sababu moja ya changamoto kubwa inayolitafuna bara letu la Afrika ni unyonyaji mkubwa unaofanywa na mataifa makubwa ya kibeberu duniani dhidi ya Afrika kwa kisingizio cha soko huria, na vile vile kukosa viongozi wenye dhamira ya dhati kupinga unyonyaji huu hata japo kwa maneno tu achilia mbali vitendo
Kukosekana viongozi shupavu wa namna hiyo kunatokana na uoga wa kupambana na mataifa makubwa hayo ya kibeberu, nayo ni kwa sababu ya nguvu kubwa za kiuchumi na kijeshi za mataifa yao,wengi tunajua viongozi wachache walio jaribu mwisho wao ulikuwaje, mfano Patrice Lumumba; Muammar Gaddafi, Thomas Sankara na wengine wengi
Binafsi napata shida sana, kuona kama Taifa Mungu katujalia kumpata kiongozi jasiri na shupavu mwenye udhubutu wa kujaribu kuangalia kinachofanywa na wawekezaji wetu hawa, kama ni sahihi ama kuna mapungufu sehemu, lakini kuna baadhi ya wanadiasa wachache kama Tundu Lissu wanaona anachofanya mh Rais ni kutafuta umaarufu wa kisiasa na sio kutetea maslahi ya Tanzania
Hapo ndio namtizima mh Lissu kama mwanasiasa, yeye kama mwanaharakati kwa siku za nyuma alipambana vikali kupinga changamoto hizo katika sekta ya madini, leo anatokea kuongozi anayejaribu kusimamia hilo anatofautiana naye sababu tu anatoka kwenye chama chenye itikadi tofauti na chama chake, kwamba akifanikiwa kwa hio itamjenga mh Rais kisiasa na hivyo kupingana na malengo makubwa ya chama chake ya kuja kushika dola siku za mbeleni
Wakati huo huo anamshutumu mh Rais kuwa alikuwa sehemu ya mfumo uliobariki sheria yetu ya madini ya mwaka 1998, ambayo hakika bila shaka ni kweli imeonekana ina mapungufu mahala
Lakini embu turejee miaka hiyo wakati muswada wa sheria hiyo unaandaliwa, mwaka 1995 mpaka 2000, mh Rais alikuwa naibu waziri wizara ya ujenzi, hivyo basi kwa nafasi yake hakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri, ambao wajumbe wake ni mawaziri kamili, ambao kumsingi miswada ya sheria hupitia huko kabla ya kupelekwa bungeni kujadiliwa
Lakini tutazame nafasi walizokuwa nazo viongozi wenzie ndani ya chama chake kwa sasa, tuanze na mh Sumaye, yeye alikuwa waziri mkuu na mh Lowassa yeye alikuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais, kimsingi hao wote wawili walishiriki kukamilifu kuandaa muswada wa sheria hiyo kuliko mh Rais Magufuli, kwani wote walukuwa wajumbe wa baraza la mawaziri la wakati huo
Nimejaribu kuonyesha yote hayo kwa lengo la kuonyesha kwa sasa si wakati muafaka wa kujaribu kutafuta nani alikosea wapi, kama taifa tunapaswa kutambua tuko kwenye vita kubwa ya kiuchumi ambayo ili tusije vita hii, umoja wetu ni lazima pasipo kujali itikadi zetu na malengo yetu ya kisiasa
Tumepata kiongozi wenye kuonesha nia ya dhati ya kukomesha unyonyaji huo, hii ni fursa kwetu sisi Watanzania kuakikisha kila mtanzania kwa nafasi yake tunamshauri mh Rais njia sahihi za kudai haki yetu katika hilo
Nitoe wito tu kwa wanasiasa wote na wa vyama vyote, hili suala si la chama chochote cha siasa hili ni letu sote kama Watanzania, hivyo tusitafute mchawi, tupambane tupate haki yetu, then baada ya hapa tukae chini kama taifa tutizame tulijikwaa wapi then tuakikishe aturudii tena makosa yetu
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika