Napata mashaka na kiwango cha elimu yetu.

Nkungulume

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
2,987
Reaction score
1,210
Habari za asubuhi hapa jamvini.
Ni matumaini yangu kuwa mmeamka salama wale ambao mpo mapuzikoni kila la kheri. Na wale ambao mnaenda kuwajibika nawatakia kazi njema.
Ni rudi kwenye mada yapata kama miezi miwili hivi nilikuwa nikisafiri kutoka Dar kwenda Lindi.

Katika siti niliyokaa alikuwepo bint mmoja ambaye kwa mjibu wa maelezo yake ilikuwa na mara ya kwanza kufika Dar. Na kwamba alikuwa amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule moja huko Masasi. Sasa kilichanishangaza tulipo pita Nangulukulu ukiaangalia upande wa mashariki bahari inaonekana.

Sasa kwa kuwa yeye alikuwa anatokea Bukoba akaniuliza hii bahari inaungana na ile ya Bukoba? Nikamwambia hapana hii ni bahari ya Hindi na lile ni ziwa Victoria.

Nikawa najiuliza hivi mtoto wa kidato cha tano bado atakuwa hajui jiografia ya inchi yake kweli? Kwa kweli bado tuna safari ndefu.
Naomba kuwasilisha.
 
ndio hivyo.alafu keshokutwa nae utasikia anajisifu saut ni bora kuliko udsm.fuata mkumbo
 
Wanafunzi wengi wanasoma ili wafaulu na Si kuelewa nini wakisomacho.

Taifa lamomonyoka sana kielimu tusipojitafakari kwa kina twafaaa
 
Ukweli nikwamba elimu yetu inachangamoto kubwa sana na changamoto hizi mtatuz ni serikali lkn hawataki kusikia uhalisia wa kiwango cha elimu yetu kua nikibovu sana badala yake wanalazimisha kuenda nazo hivo hivo!

Na watambue hiki kitu wanachokiita BRN hakimjengi mwanafunzi hata kidogo badala yake kinamdumaza, wanafunzi wa siku hizi hawafanyi mitihani wanao ifanya ni walimu kwaio usione ajabu kwa swali hilo uliloulizwa,

walimu mashuleni hawatoshelezi halafu unamtaka afundishe na afaulishe sasa anawezaje kufaulisha wakati hakufundisha kwa kiwango kinachotakiwa kutokana na kuzidiwa na vipindi! Sasa ili aonekane kafaulisha analazimika kuufanya mtihan yeye mwenyewe.
 
Usikute alikua anapima uwezo wako wa kufikiri mana kizazihiki ni hatari tupu
 
Kwa kweli serikali inabidi ijitafakari hali hii si ya kawaida maana hiyo jiografia ya darasa la pili natatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…