Naota nakula Chakula Ndotoni

Naota nakula Chakula Ndotoni

Chakwale

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Posts
1,086
Reaction score
1,601
Wakuu habari..

Kama kichwa cha habari hapo kinavyojieleza, karibu mwezi mzima sasa nimekuwa nikiota nakula chakula ndotoni na watu mbalimbali ninao wafahamu na nisiowafahamu.

Hali hiyo inanikera sana mana ukiamka asubuhi tumbo linakuwa limejaa then linakuwa kama MTU mwenye gas tumboni hata kama Jana yake usiku niwe nimelalia chai na kipande kidogo tu cha mkate.

Kingine ni kwamba nalala saana na hata nikiamka bado nakuwa mzito kuamka mwili bado unataka kubaki kitandani tofauti kabisa na mwanzo.yaan ningekuwa KE unaweza sema labda ukapime ujauzito.

Hali hii ya kuota ota ndoto za kula chakula sijui nalishwa usiku inanikosesha raha,na hivi mambo yangu hayaendi naanza kuihusisha hali hii na mambo yangu ya kipato na kiuchumi kwenda mrama.Kama kuna yeyote ameshawahi kutana na hali kama hii alikabiliana nayo VP ili kuitatua mana naona naanza kupata fikra za kishirikina sasa,ukimjulisha na sisimizi kibao wasiotaka kuondoka nymbani kwangu hata ukiwawekewa dawa za kuwauwa or kuwamwagia maji,basi imani ya mambo ya kishirikina inaongezeka.

Nakumbuka Marehem Bibi yangu nilipokuwa Mdogo aliwahi kuniambia ukiona kwako or mtaani kuna sisimizi wengi ujue hiyo ni ishara ya mwaka huo kuwa na njaa,sasa napata kigagaziko nikiunga dots za matukio.

Kwa vile humu ni kisiwa cha Maarifa na kuna wakubwa,najua ntapata Elimu ya kunisaidia iwe ya Kisayansi, Kimila,Kidini, Kiganga nk kuwa inapotokea hali kama hiyo unatakiwa ufanyaje.

Asante...
 
Wakuu habari..

Kama kichwa cha habari hapo kinavyojieleza,karibu mwezi mzima sasa nimekuwa nikiota nakula chakula ndotoni na watu mbalimbali ninao wafahamu na nisiowafahamu.

..
Chumvi ya mawe, changanya kwenye maji ogea kwa siku 21.

Chumvi nyingine weka uvungu wa kitanda, na kama imani yako haina shida na mdudu chukuwa mfupa wa kitimoto funga kwenye kitambaa weka chini ya mto, shughuri imekwisha.

Utaanza kuota upo Marekani na kina Rihanna mnagonga Champagne tu.
 
Mkuu huoni raha unashiba na hutumii pesa yako 🤣🤣🤣(just kidin)....navyofaham mm hzo ni ishara za kukurudisha nyuma kiuchumi so mpwa pambana kiimani zaid kwa maombi na sala la sivyo utaendelea kula za uso had uone dunia sio mahala salama
 
Kuna mtu aliwahi kusema, kwenye ndoto Chakula kina maana ya Maafikio au Mafanikio.

Walozi, yaani Wachawi wanatabia ya kumlisha mtu chakula usiku na kumjaza tumbo ili aridhike asitafute, aendelee kukaa kwenye ufukara.

Lengo la kukulisha ni kukushibisha ili usiendelee kutafuta, na wengi huwa Masikini.
 
Wakuu habari..

Kama kichwa cha habari hapo kinavyojieleza,karibu mwezi mzima sasa nimekuwa nikiota nakula chakula ndotoni na watu mbalimbali ninao wafahamu na nisiowafahamu.
Nilishawahi kuwa ninaota ndoto za kulishwa majani yanayotereza mdogomoni siwezi kuyameza na siwezi kuyatema mpaka niwe napakuwa Kwa mkono kutoka kinywani,na mara nyingine nilikuwa naota nalishwa nyama ya panya anayenuka hasa. Hali hii ilikuwa inanitokea Kila mwezi mara mbili,tatu hadi mara nne.

Kwa namna fulani athari ambazo nilikuwa naziona ni hizo,uvivu kupita kiasi,usingizi unaoambatana na uchovu wakati na kufeli katika harakati nyingi za kimaisha.

Kwakuwa mimi ni muislamu nilijifanyia kisomo Cha Ruqya na nilinunua dawa Fulani ni mafuta yanaitwa KIMONDO na Kuna KIMONDO NYINGINE ya kujifukiza nikatumia dawa mpaka sasa ni mwaka wa pili Alhamdulillah sijaota tena ndoto hizo. Na sio mvivu tena napiga kazi sanaaa na nashukuru kipato kimeongezeka maradufu na biashara yangu inakwenda vizuri kabisa.
 
Mkuu huoni raha unashiba na hutumii pesa yako (just kidin)....navyofaham mm hzo ni ishara za kukurudisha nyuma kiuchumi so mpwa pambana kiimani zaid kwa maombi na sala la sivyo utaendelea kula za uso had uone dunia sio mahala salama
Duuh!!Mkuu hili suala LA kunirudisha nyuma naona kama wanataka kufanikiwa hivi mana kila ninachofanya hakifanikiwi licha ya juhudi kubwa na Maarifa ninayoyafanya.Yaani sasa hivi hakuna positives kwenye kila kitu zaidi ya negatives tu.

Mshahara uliokuwa unakidhi kidogo mahitaji ya chakula sasa hivi imekuwa kinyume lazima nikope kila mwezi ili walau familia ile kwa mbinde,licha ya dilidili zingine tofauti na mshahara.

Huwa nalima Mahindi kijijini kwetu kila mwaka kwa ajili ya Chakula na mengine nauza niongeze kipato,ila mwaka huu Mahindi yote yamekauka kwa jua yakiwa kwenye mbelewele kwa kukosa Mvua.unachosema dunia kuiona chungu dalili naanza kuziona Mkuu.
 
Hiyo ndoto mbona ni nzuri tu. Itakusaidia kubana matumizi ya kununua chakula.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom