ugali wa muhogo
Member
- Jun 17, 2016
- 11
- 13
Habarini wana jamii.
Naombeni mnisaidie, nilitokea kumpenda binti mmoja ambae alikuwa mzuri sana lakini pia alikuwa na msimamo wa kimaisha pia kiimani. Alikuwa ni binti ambae hatetereshwi kirahisi tena hata ngono aliniambia hawezi kufanya kabla ya kuolewa. Nilipomdodosa zaidi aliniambia kuwa yeye bado ni bikra na kuwa kwa changamoto ambazo ameshawahi kupitia hadi sasa na hakufanya ngono inamuhakikishia kutofanya kabisa hadi kuolewa.
Nilizidi kumpenda zaidi alipokuwa akinisimulia maisha yake ya kijasiri na malengo yake ya kimaisha nikamwona kama mwanamke pekee ambaye angenifaa maishani. Ndipo nilipoamua kwa dhati kuwa tusubiriane. Yeye amemaliza certificate ya ualimu mwaka huu na mimi niko mwaka wa tatu nachukua degree ya uhandisi.
Tatizo kubwa lililojitokeza tokea mwanzo ni tofauti zetu za kidini. Yeye ni Msabato aliyebadili toka ukatoliki na amefundishwa misimamo mingi ya kidini na mimi nilikuwa Mkatoliki. Nilimshauri kubadili dini na kuwa mkatoliki lakini alikataa kabisa kurudi ukatoliki. Kwa kuwa nilimpenda sana na sikuwa tayari kumuacha nilibadili dini mimi, nikabatizwa rasmi kuwa Msabato.
Maisha yakaendelea, nilimpenda kweli na hata alipopatwa na shida especially ya kiuchumi nilijitahidi kuitatua kadiri ya uwezo wangu. Tulikuwa tunasali kanisa moja, akaanza kufahamika sana kanisani kutokana na kujituma kwake kwa mambo ya ibada. Sikujua ni shetani gani aliyepita kati yetu. Baada ya mda mambo yalibadilika. Nikawa nampigia simu hapokei lakini pia hata akipokea anaongea kwa kifupi.
Nilimvumilia nikajipa moyo labda ndo hivyo mabinti walivyo. Siku moja aliniita kwamba ana mazungumzo na mimi, nilikubali tukapanga kukutana. Katika mazungumzo yake alikuwa anataka tuvunje ahadi tulizowekeana za kuja kuoana kwa kigezo kuwa yeye bado ana mpango wa kusoma mda mrefu kwa hiyo itakuwa vigumu kusubiriana mda wote huo. Sikuona kuwa ni sababu ya maana kwangu lakini aliendelea kunisihi kuwa yeye hatoweza kuwa kwenye mahusiano kwa mda wote huo.
Mwisho tulisitisha mahusiano ingawa sikupenda. Tokea tuachane mwezi umepita sasa, najitahidi nidumu katika imani lakini najikuta kila siku imani inashuka kiwango. Najihisi mpweke na mnyonge hata kanisani naona hakuna umuhimu.
Naombeni mnisaidie ushauri.