Hivi karibuni Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), ilitangaza kwa mbwembwe wiki iliyopita kuwa Bia aina ya Castle Light ingeuzwa kwa Tshs.2,000 badala ya 2,500. Hata hivyo nimegundua kuwa Bar nyingi bado zinauza kinywaji husika kwa 2,500. Ukiwauliza wenye Bar unaambiwa distributors bado wana stock ya zamani. TBL hawakujua kiwango cha Bia hizo kilichopo sokoni?. Mbaya zaidi tangazo husika lilisema bei mpya (elekezi) ingeanza kesho yake. Huu ni uhuni sasa. Ngoja nihamie kwenye Serengeti ndogo sasa.