Naombeni ushauri wenu juu ya CWT wana JF!

Naombeni ushauri wenu juu ya CWT wana JF!

Joined
Jun 30, 2013
Posts
21
Reaction score
14
Ndugu zangu wana JF, mimi ni Mwalimu Idara ya Sekondari katika Wilaya X.Tarehe 20 Januari 2014 nilichaguliwa kwa kura nyingi kuwa mwakilishi wa Chama cha Walimu idara ya Sekondari Wilaya katika uchaguzi wa kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi.

Tangu siku hiyo ya uchaguzi sijawahi kushirikishwa katika shughuli yoyote ile ya chama ikiwa ni pamoja na kuambiwa majukumu na mipaka yangu ya kazi hiyo ya uwakilishi,sijui nianzie wapi na niishie wapi katika kuwawakilisha wapiga kura wangu katika chama hicho cha walimu.

Chama kiko mikononi mwa watu watatu tu ambao ni Katibu wa Wilaya,Mwenyekiti na Mhazini.

Je Wana jf,katika mazingira kama haya kuna sababu yoyote ya mimi kuendelea na nafasi hiyo ilhali siitendei haki? Naombeni ushauri wenu!
 
Ushauri wangu ni huu kwamba usiachie ngazi, komaa hadi mfumo ulioukuta ubadilike ili haki za waliokuchagua zipatikane bila mizengwe. Ukijitoa utakua umewaachia nyani shamba la mahindi.
 
hicho chama ni cha waalimu wa shule ya msingi wanawabagua sana waalimu wa sekondari ni muda wenu kuanzisha chama chenu waalimu wa sekondari
 
Ndugu zangu wana JF, mimi ni Mwalimu Idara ya Sekondari katika Wilaya X.Tarehe 20 Januari 2014 nilichaguliwa kwa kura nyingi kuwa mwakilishi wa Chama cha Walimu idara ya Sekondari Wilaya katika uchaguzi wa kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi.

Tangu siku hiyo ya uchaguzi sijawahi kushirikishwa katika shughuli yoyote ile ya chama ikiwa ni pamoja na kuambiwa majukumu na mipaka yangu ya kazi hiyo ya uwakilishi,sijui nianzie wapi na niishie wapi katika kuwawakilisha wapiga kura wangu katika chama hicho cha walimu.

Chama kiko mikononi mwa watu watatu tu ambao ni Katibu wa Wilaya,Mwenyekiti na Mhazini.

Je Wana jf,katika mazingira kama haya kuna sababu yoyote ya mimi kuendelea na nafasi hiyo ilhali siitendei haki? Naombeni ushauri wenu!
Kama ulichaguliwa kwa kura nyingi inakuwaje unawagwaya watu watatu? Naomba uelewe kuwa umechaguliwa ili ulete mabadiliko. Ukiona mambo hayaendi, itisha kikao cha waliokuchagua mpeane modality. Ukiaminiwa na watu, jitume.
 
Dah!
Sijui hata kwanini walikuchagua maaana hata hujui cha kufanya.Uliomba kura?Kama ndiyo je ulihaidi kufanya yepi?
Kwanini usianze na hayo?
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Unauliza eti hujui uanzie wapi halafu uishie wapi....!?
Mwalimu....!?
Hivi,ulichaguliwa ili iweje?
Majibu ya ..."ili"..(yaani hapo juu) ndiyo kazi yako.
Anzia cwt hapo hapo na uishie mahakamani.
 
Kama kweli hujui pa kuanzia na pa kuishia ni shida kwa wote yaani wewe na unaowawakilisha. Na ndio maana wanaojua pa kuanzia na pa kumalizia wapo ofisini wanatwanga 2% ya salary yako. Amkeni mliochaguliwa mkatii kiu ya walimu wanyonge. Na niwaulize walimu, mtakuwa wanyonge hadi lini? Hivi ningekuwa mwalimu ningewahamasisha wenzangu na kuwatoa wakurugenzi kwenye maofisi yao pindi watafunapo mishahara yetu!
 
Cwt ni wezi sijui kwa nini bado mnakomaa kuendelea kuwa nao kwenye hii michakato.
 
Back
Top Bottom