Mimi niko Mz. Niionavyo Chalinze nikipita kwenda Dar,inakua kwa kasi. Hivyo population inakua kwa kasi. Kuna vihoteli na mama ntilie wengi. Pia kuna watembeza mayai na nyama ya kukuk n.k. Katika mazingira hayo, nenda pale ,fanya utafiti mdogo wa kujua sources yaani vyanzo vya bidhaa zao,bei,na msimu wanaouza sana. Hii inaitwa "market research" yaani utafiti wa soko. Pia unaweza kwenda hadi Mlandizi, na maeneo mengine jirani,hata Dar. Na ili ufaidi eneo lako,na pesa ikue kwa haraka,anza na miradi inayoitwa "quick win projects" yaani inayochukua muda mfupi lakini ina faida.
Utakachokipata katika utafiti wako kama nilivyokueleza hapo juu,anza nacho. Mfano,ingekuwa mimi nimegundua kuwa mazao ya kuku na mbogamboga ndiyo mahitaji makuu,ningeanza na hivyo (gawa eneo mara 2 au 3). Jua ukiwa na miradi miwili tofauti kuna faida! Unapunguza hasara kama kutakuwa na janga (risk) kwa mradi mmoja,na pili miradi itabebana. mfano, ukianza na mchicha au nyanya,utapata fedha ya kuendeleza kuku na kinyume chake. Ziko post nyingi humu kuhusu ufugaji wa kuku na mbogamboga. Pia nashauri kabla ya kuanza kwa kila sekta,mwone mtaalamu wa sekta hiyo aliyekaribu aone shamba,akushauri na uwe karibu naye.
Naamini nimetoa ushauri wa jumla. Utakachamua baada ya utafiti (market research) tupe mrejesho,ninaweza kukushauri vizuri kwenye business plan (Mpango wa biashara)