Naombeni ushauri kuhusu biashara ya daladala

Vvip

Senior Member
Joined
Apr 7, 2016
Posts
190
Reaction score
87
Habari zenu ndugu zangu natumaini mko salama natumaini mko poa,naombeni mawazo yenu ktk hili nimekuwa nikitamani kufanya biashara ya daladala na matamanio yangu naona yanafikia ktk lengo ss nimefikiria mengi ila nimeona nijitose tu ila dereva ni mimi mwenyewe je NITAFIKA?????,Mawazo yenu jamani.
 
Inahitaji usimamizi wa karibu sana. Inahitaji dereva muaminifu. Kama unanunua dala dala ambayo ilishatumika bora uache kabisa (Madereva wengi wanapenda zilizochoka ili wakudanganye gari...ilikuwa gereji). Kama umeiagizia hiyo fanya ila uakikishe gereji upeleke wewe mwenyewe lasivyo watakubadilishia vitu. Pia uwe na fundi muaminifu kwa ajili ya services.
 
Asante kwa ushauri wako ila dereva ni mimi mwenyewe hapo vp???.
 
Habari zenu ndugu zangu natumaini mko salama natumaini mko poa,naombeni mawazo yenu ktk hili nimekuwa nikitamani kufanya biashara ya daladala na matamanio yangu naona yanafikia ktk lengo ss nimefikiria mengi ila nimeona nijitose tu ila dereva ni mimi mwenyewe je NITAFIKA?????,Mawazo yenu jamani.
Bora uwe konda.
 
Asante kwa ushauri wako ila dereva ni mimi mwenyewe hapo vp???.
Ushauri:
  1. Uwe konda, yaani kusanya hela mwenyewe (ukimuachia mwingine anaweza kuchonga tiketi, halafu ukashangaa tiketi zimetoka chache na wakati mmefanya kazi kubwa).
  2. Ukienda gereji usikubali kuacha gari, litengenezwe ukiwepo (Tena kwa Dar ndiyo wezi wezi sana mafundi na ni wahuni na waongo sana).
  3. Hakikisha unafungua account bank (kila ukipata hiyo hela hakikisha unaiweka bank siku inayofuata, usirundike hela nyumbani).
  4. Hakikisha hela unayoweka bank iwe faida tu, yaani toa gharama zako zote.
  5. Jiwekee malengo ya muda mrefu (yaani uwe kama unaanza kidato cha kwanza mpaka cha nne), kazi yako iwe kuweka na kukusanya hela. Ila ikiwa nyingi kabla ya hiyo minne unaweza kuwekeza kwenye kitu ambacho unausimamizi nacho wa moja kwa moja
 
Mawazo mazuri sana yaani niwe kama naanza kidato cha kwanza,kizuri zaidi ni hapo kwenye malengo ya muda mrefu.
 
Yote waliyosema wadau hapo juu yana maana. Na kuna mengi zaidi unapaswa kuyafahamu kuhusu hii biashara. Ingawaje ya msingi ni machache sana na ukikosea hapo ndo linakuja neno "PASUA KICHWA". Kwa ufupi ni biashara nzuri na mimi binafsi naifanya. Nitarudi baadae kidogo kukupa dondoo.

Update:

Mimi binafsi niliingia katika biashara ya usafirishaji (daladala) kutokana na kuwa na hobby nayo. Niliamini kila kitu nitakijua mbele kwa mbele nikiwa ndani tayari kwasababu kila niliojaribu kuwadadisi kuhusu biashara hii walinikatisha tamaa na wachache walininia moyo. Nikaona isiwe tabu, acha niingie mwenyewe nijionee. Nilipata elimu ya kutosha na nikafikia uamuzi wa kwenda kufanya practical. Nilinunua gari yangu ya kwanza (hiace) kwa kuagiza mwenyewe direct toka Japan na nikazama barabarani. Kufika barabarani ikawa kama ndo nimeanza shule kwani kinachozungumzwa na kinachoendelea kiuhalisia ni vitu viwili tofauti. Baada ya miezi kama sita nikawa nimehitimu kozi na kuweka misingi ya kusonga mbele na nilimudu, huu mwaka wa nne.

Zingatia haya:

1. Nunua gari kwa kuagiza mwenyewe toka Japan, usinunue kwa mtu, hatakama ni nusu ya bei ya kuagiza. Zingatia gari nzuri na pia kulingana na malengo yako kama ni ya muda mfupi au mrefu. Ukiwa na gari nzuri na utunzaji mzuri, garage utakuwa unapasikia tuu.

2. Kuwa konda katika gari yako ya kwanza au kuwa dereva. Utajua ulaji mafuta, wastani wa umbali inaotembea kwa siku, hela inayolaza kwa siku na barabara ilivyo.

3. Tokea ikiwa mpya mikononi mwako, usiruhusu fundi yeyote aifanyie service au kurekebisha chochote zaidi ya mmoja unayemwamini na utakayeingia mkataba nae kwa kumlipa kwa mwezi hatakama gari haijaenda garage.

4. Hela inayopatikana igawe mara 3 katika uwiano wa 2:3:5 kama unataka ufikie malengo ndani ya muda mfupi. Huo uwiano ni Mshahara wako, Matengenezo, Uchakavu wa gari. Mfano; Kwa siku kama gari inalaza 100,000tsh; ukitenga 20,000tsh kama Mshahara wako, 30,000tsh kama Matengenezo na 50,000 uchakavu wa gari huo ni uwiano wa 2:3:5

5. Tafsiri ya gharama za uchakavu iko hivi: Gari kama ilikugharimu 30,000,000tsh kuinunua hadi kuiweka barabarani, basi ukitunza hela ya uchakavu 50,000 kila siku ambayo gari imefanya kazi, utawezakuwa umetunza 30,000,000 ndani ya miaka miwili. Hela hiyo itakuwezesha kununua nyingine zikawa mbili. Ila kama una majukumu mengi na unaona mshahara wa 20,000 kwa siku haukutoshi, basi weka malengo yako ndani ya muda mrefu kidogo ila isizidi miaka mitatu. Hapo utaongeza mshahara na kupunguza uchakavu. Mfano uwiano wa (4:3:3). Mshahara 40,000tsh, matengenezo(uendeshaji) 30,000 na uchakavu 30,000tsh. Baada ya takribani miaka mitatu utakuwa umeweza kurudisha hela uliyonunulia na ukaagiza gari nyingine.

6. Hela ya uchakavu wa gari nakushauri uitunze katika dola na siyo tsh. Fungua akaunti ya dola na uwe unatunza humo. Ukiwa na tsh, nenda kanunue dola na u deposit katika hiyo akaunti.

7. Matumizi yako yasizidi mshahara wako, labda kama umeingiza ziada au umekopa dola ktk akaunti ya gari.

8. Hela ya matengenezo itunze kivyake na ya uchakavu kivyake*. Hapa kwenye uchakavu ndipo wengi huwa tunakosea na matokeo yake unakuta mtu ameanza biashara vizuri na gari nzuri ila mwisho wa siku miaka inapita na gari imechakaa na hawezi hata kununua nyingine hadi anaiegesha juu ya mawe au kila siku kushinda garage.

9. Hela ya matengenezo iheshimiwe na gari ihudumiwe kwa fungu hilo na siivinginevyo. Hii inajumuisha gharama zote za uendeshaji wa biashara yako kama vile malipo ya fundi kwa mwezi, karatasi, vibali, vipuri, oil, filters, brake pads, brake shoes, matairi etc.

10. Dereva mlipe kwa wiki. Mimi madereva wangu huwa wanafanya kazi siku 5 kwa wiki(mfano J3-Ijumaa), kisha siku ya sita ni yake. Konda analipwa kwa siku na dereva. Siku ya saba huwa ni off ambayo hutumika kupeleka gari service kama inahitajika au kama haihitajiki, basi dereva afanye kazi kama anajisikia kwa kiasi mtakachokubaliana akuletee kwa siku hiyo. Gari ya abiria servisse siyo mpaka iharibike, ni pamoja na kuchekiwa mifumo ya kiusalama hasa braking system, matairi, suspension na steering, bila kusahau mfumo wa umeme unaojumuisha taa zote na indicators pamoja na honi. Ajali nyingi chanzo huwa ni hivyo vitu ukiondoa uzembe wa dereva. Pia kucheki level ya fluids kama engine oil, gear box oil, differential, coolant/maji system. Fundi si unamlipa? Peleka gari anytime. Tena atatengeneza vizuri usirudi rudi garage.

11. Weka GPS CarTrack kwenye gari yako, itakusaidia kui monitor popote pale ulipo kupitia simu yako ya mkononi na hivyo dereva hawezi na hatathubutu kukudanganya chochote maana unaiona ilipo na kama inatembea pia unaona ikisogea na pia eneo alipo.

Nilianzaga na daladala moja, na nikajiwekea huo utaratibu, sasahivi zipo kadhaa na ninauwezo wa kuongeza moja au zaidi kila mwaka. Mwanzo ndo huwa mgumu, ila zikishakuwa mbili, makusanyo yanakuwa mara mbili na zikiwa tatu hivyo hivyo yanaongezeka huku gari ya kwanza ikiwa imechoka hivyo unamsukumia mtu anayehitaji kisha unajazia unaagiza mpya. Ilimradi uwe na nidhamu ya pesa na uichukulie kama ajira yako.

Cc @
Investor I
 
Hiyo biashara imekuwa ngumu sana asaivi sio siri...km unanua mpya ujue ni kuanzia mil 45 na kuendelea, hesabu ni laki kwa siku...kuna vyeti (notification) hatari yaani asaivi mapato ya nchi yanatokea hapo, ila muombe Mungu
 
Habari zenu ndugu zangu natumaini mko salama natumaini mko poa,naombeni mawazo yenu ktk hili nimekuwa nikitamani kufanya biashara ya daladala na matamanio yangu naona yanafikia ktk lengo ss nimefikiria mengi ila nimeona nijitose tu ila dereva ni mimi mwenyewe je NITAFIKA?????,Mawazo yenu jamani.
kaa mbali usiguse!
 
Asante kaka nashukuru kwa ushauri mzuri umenipa nguvu zaidi ,kama vp urudi basi tuzungumze pls.
 
Hiyo biashara imekuwa ngumu sana asaivi sio siri...km unanua mpya ujue ni kuanzia mil 45 na kuendelea, hesabu ni laki kwa siku...kuna vyeti (notification) hatari yaani asaivi mapato ya nchi yanatokea hapo, ila muombe Mungu
Asante kaka kwa ushauri wako,ila mi nanunua toyota hiace ni used nje.
 
Ushauri:
  1. Uwe konda, yaani kusanya hela mwenyewe (ukimuachia mwingine anaweza kuchonga tiketi, halafu ukashangaa tiketi zimetoka chache na wakati mmefanya kazi kubwa).
  2. Ukienda gereji usikubali kuacha gari, litengenezwe ukiwepo (Tena kwa Dar ndiyo wezi wezi sana mafundi na ni wahuni na waongo sana).
  3. Hakikisha unafungua account bank (kila ukipata hiyo hela hakikisha unaiweka bank siku inayofuata, usirundike hela nyumbani).
  4. Hakikisha hela unayoweka bank iwe faida tu, yaani toa gharama zako zote.
  5. Jiwekee malengo ya muda mrefu (yaani uwe kama unaanza kidato cha kwanza mpaka cha nne), kazi yako iwe kuweka na kukusanya hela. Ila ikiwa nyingi kabla ya hiyo minne unaweza kuwekeza kwenye kitu ambacho unausimamizi nacho wa moja kwa moja
tafuta fundi mmoja ingia naye mkataba, gari hata likiharibikia busa sio mlandizi anataliwa akalitengeneze. ukiruhusu dereva kupeleka gereji anazotaka basi itakula kwako. na habari zote za ubovu wa gari zinataliwa ziletwe na fundi na sio dereva.
 
Yote waliyosema wadau hapo juu yana maana. Na kuna mengi zaidi unapaswa kuyafahamu kuhusu hii biashara. Ingawaje ya msingi ni machache sana na ukikosea hapo ndo linakuja neno "PASUA KICHWA". Kwa ufupi ni biashara nzuri na mimi binafsi naifanya. Nitarudi baadae kidogo kukupa dondoo.

Update:

Mimi binafsi niliingia katika biashara ya usafirishaji (daladala) kutokana na kuwa na hobby nayo. Niliamini kila kitu nitakijua mbele kwa mbele nikiwa ndani tayari kwasababu kila niliojaribu kuwadadisi kuhusu biashara hii walinikatisha tamaa na wachache walininia moyo. Nikaona isiwe tabu, acha niingie mwenyewe nijionee. Nilipata elimu ya kutosha na nikafikia uamuzi wa kwenda kufanya practical. Nilinunua gari yangu ya kwanza (hiace) kwa kuagiza mwenyewe direct toka Japan na nikazama barabarani. Kufika barabarani ikawa kama ndo nimeanza shule kwani kinachozungumzwa na kinachoendelea kiuhalisia ni vitu viwili tofauti. Baada ya miezi kama sita nikawa nimehitimu kozi na kuweka misingi ya kusonga mbele na nilimudu, huu mwaka wa nne.

Zingatia haya:

1. Nunua gari kwa kuagiza mwenyewe toka Japan, usinunue kwa mtu, hatakama ni nusu ya bei ya kuagiza. Zingatia gari nzuri na pia kulingana na malengo yako kama ni ya muda mfupi au mrefu. Ukiwa na gari nzuri na utunzaji mzuri, garage utakuwa unapasikia tuu.

2. Kuwa konda katika gari yako ya kwanza au kuwa dereva. Utajua ulaji mafuta, wastani wa umbali inaotembea kwa siku, hela inayolaza kwa siku na barabara ilivyo.

3. Tokea ikiwa mpya mikononi mwako, usiruhusu fundi yeyote aifanyie service au kurekebisha chochote zaidi ya mmoja unayemwamini na utakayeingia mkataba nae kwa kumlipa kwa mwezi hatakama gari haijaenda garage.

4. Hela inayopatikana igawe mara 3 katika uwiano wa 2:3:5 kama unataka ufikie malengo ndani ya muda mfupi. Huo uwiano ni Mshahara wako, Matengenezo, Uchakavu wa gari. Mfano; Kwa siku kama gari inalaza 100,000tsh; ukitenga 20,000tsh kama Mshahara wako, 30,000tsh kama Matengenezo na 50,000 uchakavu wa gari huo ni uwiano wa 2:3:5

5. Tafsiri ya gharama za uchakavu iko hivi: Gari kama ilikugharimu 30,000,000tsh kuinunua hadi kuiweka barabarani, basi ukitunza hela ya uchakavu 50,000 kila siku ambayo gari imefanya kazi, utawezakuwa umetunza 30,000,000 ndani ya miaka miwili. Hela hiyo itakuwezesha kununua nyingine zikawa mbili. Ila kama una majukumu mengi na unaona mshahara wa 20,000 kwa siku haukutoshi, basi weka malengo yako ndani ya muda mrefu kidogo ila isizidi miaka mitatu. Hapo utaongeza mshahara na kupunguza uchakavu. Mfano uwiano wa (4:3:3). Mshahara 40,000tsh, matengenezo(uendeshaji) 30,000 na uchakavu 30,000tsh. Baada ya takribani miaka mitatu utakuwa umeweza kurudisha hela uliyonunulia na ukaagiza gari nyingine.

6. Hela ya uchakavu wa gari nakushauri uitunze katika dola na siyo tsh. Fungua akaunti ya dola na uwe unatunza humo. Ukiwa na tsh, nenda kanunue dola na u deposit katika hiyo akaunti.

7. Matumizi yako yasizidi mshahara wako, labda kama umeingiza ziada au umekopa dola ktk akaunti ya gari.

8. Hela ya matengenezo itunze kivyake na ya uchakavu kivyake*. Hapa kwenye uchakavu ndipo wengi huwa tunakosea na matokeo yake unakuta mtu ameanza biashara vizuri na gari nzuri ila mwisho wa siku miaka inapita na gari imechakaa na hawezi hata kununua nyingine hadi anaiegesha juu ya mawe au kila siku kushinda garage.

9. Hela ya matengenezo iheshimiwe na gari ihudumiwe kwa fungu hilo na siivinginevyo. Hii inajumuisha gharama zote za uendeshaji wa biashara yako kama vile malipo ya fundi kwa mwezi, karatasi, vibali, vipuri, oil, filters, brake pads, brake shoes, matairi etc.

10. Dereva mlipe kwa wiki. Mimi madereva wangu huwa wanafanya kazi siku 5 kwa wiki(mfano J3-Ijumaa), kisha siku ya sita ni yake. Konda analipwa kwa siku na dereva. Siku ya saba huwa ni off ambayo hutumika kupeleka gari service kama inahitajika au kama haihitajiki, basi dereva afanye kazi kama anajisikia kwa kiasi mtakachokubaliana akuletee kwa siku hiyo. Gari ya abiria servisse siyo mpaka iharibike, ni pamoja na kuchekiwa mifumo ya kiusalama hasa braking system, matairi, suspension na steering, bila kusahau mfumo wa umeme unaojumuisha taa zote na indicators pamoja na honi. Ajali nyingi chanzo huwa ni hivyo vitu ukiondoa uzembe wa dereva. Pia kucheki level ya fluids kama engine oil, gear box oil, differential, coolant/maji system. Fundi si unamlipa? Peleka gari anytime. Tena atatengeneza vizuri usirudi rudi garage.

11. Weka GPS CarTrack kwenye gari yako, itakusaidia kui monitor popote pale ulipo kupitia simu yako ya mkononi na hivyo dereva hawezi na hatathubutu kukudanganya chochote maana unaiona ilipo na kama inatembea pia unaona ikisogea na pia eneo alipo.

Nilianzaga na daladala moja, na nikajiwekea huo utaratibu, sasahivi zipo kadhaa na ninauwezo wa kuongeza moja au zaidi kila mwaka. Mwanzo ndo huwa mgumu, ila zikishakuwa mbili, makusanyo yanakuwa mara mbili na zikiwa tatu hivyo hivyo yanaongezeka huku gari ya kwanza ikiwa imechoka hivyo unamsukumia mtu anayehitaji kisha unajazia unaagiza mpya. Ilimradi uwe na nidhamu ya pesa na uichukulie kama ajira yako.

Cc @
Investor I
Shukran kiongozi
 
Habari zenu ndugu zangu natumaini mko salama natumaini mko poa,naombeni mawazo yenu ktk hili nimekuwa nikitamani kufanya biashara ya daladala na matamanio yangu naona yanafikia ktk lengo ss nimefikiria mengi ila nimeona nijitose tu ila dereva ni mimi mwenyewe je NITAFIKA?????,Mawazo yenu jamani.
Biashara ya nyanya hiyo dereva Mwenyewe sawa! Konda ale, tragic p ale, gari Ile, serekali Ile, teja ale...halafu wewe nawe ule utaongea kwa lugha muda si mrefu
 
Mkuu ulitoa maelezo mazuri sana sana, kwa Dar es salaam ni aina gani ya gari inafaa kulingana na experience yako??
 
Safi sana Great thinker.... Binafsi nimepata kitu cha kujifunza hapa.. Mungu akubariki katika biashara yako na ikawe na mafanikio tele..

I salute JMF
 
Back
Top Bottom