Naombeni msaada wenu wanaJF wenzangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni msaada wenu wanaJF wenzangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by KIBURUDISHO, Jul 5, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kipindi cha siku za usoni kati ya mwaka 2004 na5 niliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada mmoja lakini baadae baada ya kumgundua ni mbwa mwitu aliyejitanda ngozi ya kondoo niliamua kuachana naye.Kwa ujumla tabia yake ilikuwa mbaya!!!!!. Kwa sasa ninaye mpenzi wangu ninayempenda sana anayejiheshimu na tunathaminiana.Hivyo basi ktk hali isiyokuwa ya kawaida kwa siku chache zilizopita nimegundua kuwa mpenzi wangu huyu wa sasa ameanza urafiki na yule dada tuliyeachana naye hapo awali.Nikizikumbuka tabia za awali za yule dada zisizokuwa na chembe ya staha nipo tayari kuachana na huyu mpenzi wangu endapo nitakapomweleza juu ya urafiki wao asikubali kuachana naye. NAOMBA nieleweke wazi kuwa simkatalii urafiki wake na huyo dada kwa sababu niliwahi kuwa naye la hasha!!!!!!
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Cha msingi ni kumweleza ukweli juu ya mahusiano yako ya awali na huyo dada na kwa nini uliachana naye. Sababu za kuachana naye ndo hizo zinazokufanya usipende awe na urafiki naye.....
   
 3. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  uliwahi kumweleza kuwa ulikuwa na mahusiano na yule dada?
  Kama hukumkosea huyo mpenzi wako wa zamani wala hukumfanyia kitu kibaya wasiwasi wa nini
  mpaka unasema akiendeleza urafiki na huyu mpenz wako wasasa unaweza nae kuachana nae,
  je, kuna uhusiano gani kati ya urafiki wao na mapenzi yenu?
  kama kweli mnapendana kwa dhati hilo haliwezi kukufanya utengane na huyo mpenz wako lbd kama una jingine
   
 4. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hivi wewe utakuwa unajisikia vizuri sana kama mkeo unayempenda kwa dhati anakuwa na urafiki na madada wanaojiuza????? Eti kisa tu unampenda kwa dhati?.Upo nyumbani wanakuja hao rafiki zake wanaanza kupiga story na mkeo juu ya biashara yao ya kujiuza!!!!!!!!!!!!????????????
   
 5. H

  Hayati Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafuta muda mzuri kumuelewesha sabbu za kutaka asiwe rafiki ykhuyo msichana tafadhali tumia busara na maneno laini kwani inaweza badaye kusababisha kuachana.
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  mweleze huyo mpenzi wako kuhusu huyo mdada. Muweke wazi kuwa mliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, pia mwambie why ulisitisha mahusiano. Hope atakuelewa.
   
 7. charger

  charger JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,324
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mwambie tu ukweli na jinsi unavyojisikia maana hapo kuna mashaka juu ya huo urafiki usikute huyo aliye achwa anataka amwingize mkenge na mwenzie kwa kuona labda anafaidi.Mtu akikupenda kwa dhati yupo radhi a sucrifice mambo yake ikiwa yanaonekana kuhatarisha uhusiano wenu.
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,658
  Trophy Points: 280
  Una matatizo mawili!La kwanza unaogopa matokeo ya urafiki wao kuwa mabaya kitu ambacho huwezi kubadili,hivyo ni ujinga kuogopa jambo ambalo liko nje ya uwezo wako,pia fahamu hizo ni hisia zako tu sio kitu halisi,pengine urafiki wao ni wa kawaida,jambo la pili,hauko tayari kumuacha,unampenda bado,kitendo cha kutaka ushauri hapa kinaashiria kuwa hujui cha kufanya au hauko tayari kufanya unachofikiria,so unayosema kuwa uko tayari kumuacha sio kweli,jikague vizuri,acha kuogopa mawazo!Kaa na mpenzi wako!
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mpige stop haraka huyo mpenzi wako. Na mwambie kabisa achague either you au huyo X. Ninachoona ni kuwa huyo X atakuwa na hidden agenda. Lazima akuharibie. Yani kwenye wasichana wote ameona awe na urafiki na girlfriend wa X wake. Lazima atakuwa na mission ya kukukomoa.
   
 10. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,687
  Likes Received: 8,221
  Trophy Points: 280
  "Birds of a feather, flock together." - Wahenga
   
 11. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Rafiki wa adui yako ni adui yako.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mbona issue ndogo tu hiyo. zungumza na mpenzi wako, mueleze kinagaubaga a to z kuhusu ex wako kwa mwanamke mwerevu atajua cha kufanya
   
 13. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mweleze hutaki awe na mazoea na huyo x wako.kama ni mwelewa atakusikia.
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red? Mmmh kama ya kutunga hivi.
   
 15. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #15
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  ukisema siku za usoni maana yake ni siku zijazo au siku za mbeleni mkuu...kuhusu huyo mpenzi wako nakushauri umpe ukweli kuhusu huyo X wako ili ajue ana deal na mtu wa aina gani.ukiona haelewi somo jua tabia zao zinaweza kuwa zinafanana kama mkuu Mentor alivyosema kwamba ndege wanaofanana huruka pamoja.
   
 16. MaVa

  MaVa Member

  #16
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwakweli km kweli unamfahamu huyo dada hana tabia inayofurahisha, mwambie tu huyo sugarbanana wako kuwa hutaki awe na mazoea na huyo dada...km kweli anakupenda na mnasikilizana atakuelewa na mambo yataisha!
   
 17. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Asanteni sana kwa ushauri wenu nimekwishaufanyia kazi na yeye mwenyewe amekili kweli niliyomwambia juu ya huyo rafiki ni ya kweli ,na hata yeye mwenyewe ameniambia tayari alikuwa amekwishaambiwa na rafiki yake mwingine juu ya tabia mbaya isiyofaa toka kwa huyo aliyekuwa rafikiake.
   
Loading...