Naombeni mnisaidie ndugu yenu.

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Hili tatizo nimekuwa tangu nilipoweza kuongea na wadada. Limekuwa likinisumbua sana na kunifanya nikorofishane na watu kufikia hatua ya kutokuongea.

Tatizo lenyewe liko hivi: Kuna wakati namuona mdada nampenda kwelikweli...nafanya mpango wa kuwa karibu nae napata mawasiliano yake na baadae namtongoza.

Wengi niliowatongoza huwa wanakataa lakini navyozidi kukaza wanakubali kuwa na mimi. Tatizo linaanza wakishakubali.

Roho mchafu ananiingia naanza kuwaona kama vile sio sehemu ya mwili wangu. Yaani naanza kuona ukubwa wa tumbo, uwembamba wa miguu na vitu kama hivyo.

Kinachofuata ninaanza kukata maasiliano nao. Na baadae nawapotezea kabisa. Mbaya zaidi nikishaachana nao huwa wanaolewa tena na waume wanaojitambua na wenye maisha mazuri tu.

Huyu roho mchafu huwa ananisumbua zaidi pale ikitokea binti kanielewa yeye na kuanza kujipitishapitisha. Huyu roho huwa ananiruhusu nimkubalie...nikishamkubalia anazamisha mizizi yake ya upendo kwangu...na badae roho ya kumkataa inaanza.

Jamani najua JF kuna watu wanauzoefu na hali kama hii. Ntashukuru nikipata msaada wa haraka.

Tatizo linaweza kuwa ni nini? Nimechoka sasa kuwa kwenye mahusiano yenye mwenendo kama huo na Mimi napenda niwe na msichana ntakayempenda kwa dhati na kudumu nae angalau hata mwaka na nusu.

Ikitokea sitapata suluhisho JF, sitajiua ila nitaachana na mapenzi naenda chuo kikuu kuongeza ma-digirii.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hali ya kawaida tu. Utaendelea hivyohivyo mpaka utakapokuja kugundua kuwa hakuna mtu aliyekamilika kwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom