Naombeni mnijuze kuhusu TALA FOUNDATION kabla sijajilipua

Na pia, hiyo namba ya simu haisomi jina ulilopewa; laini imesajiliwa kwa jina la kike, unaewasiliana anaitwa Samwel! WTFFFFF!!
 
Abuu Said mzee unataka kuibiwa kijinga tu, kopa kwenye App angalau unaona wana hela unakopeshwa. Usiibiwe na matapeli wa WhatsApp na Facebook yaani ukiona tu Facebook au WhatsApp au mtandao wa kijamii kimbia hata upatu wa kwenye magroup ya WhatsApp na watu usiowajua na wa mbali usithubutu matapeli watapokea kwanza halafu watawaachia group na kuvunja lines zao.
 
Tala niliyoikopa sana kipindi cha nyuma ni ile ambayo hatua zote unazifanya kwa app yao pasipo hata kusikia sauti ya mhusika wa tala,pakiwa na shida mnamalizana kwenye email kwa mwezi walikuwa wakichaji rate ya 20% pasipo hata kunitaka niweke akiba kwanza,na kadri nilivyokuwa nikiwalipa kwa wakati ndivyo walivyokuwa nikiongezewa kiwango cha kukopa,nakumbuka nilifikia kiwango cha kukopa hadi Tsh. 500,000 niliumia sana hawa jamaa kufunga biashara yao TANZANIA.
Ila kwa tala hiyo ya mleta uzi sijajua ni ya namna gani!
 
Mzee hao sio TALA ni matapeli shtuka unaibiwa wewe ni heri utumie branch ambao bado wapo hao TALA walisha acha kutoa huduma tz
 
Unapigwa mkuu kama uko karibu waambie unataka kuipeleka hiyo 100k physically.
 
kipindi wanafunga miaka ya nyuma, TALA walipigwa sana, wanakopwa wadau hawarudishi
naona wamekuja ku rematch, kurudisha cha kwao, na naona OP tayari ushaelekea Qibla tayari kuchinjwa
 
Back
Top Bottom