dontgiveup
Member
- Nov 10, 2014
- 22
- 5
Habari wana JamiiForums. Nina mchumba mwanajeshi ambaye kwa sasa yupo mkoa tofauti na mimi.
Uchumba wetu una miaka miwili sasa.
Mwanzoni tulikuwa tunawasiliana vizuri lakini ghafla mawasiliano yakawa magumu kwa upande wake, kwani wakati mwingine nikimpigia simu hapokei na nikimtumia meseji anajibu kwa wakati anaojisikia yeye.
Nikimuuliza kwa nini anafanya hivyo anajibu kuwa yupo bize na kazi, na ninapomuuliza kuhusu hatima ya mahusiano yetu, ananiambia kuwa yeye bado ananipenda na anachofahamu ni kwamaba mimi ndo mkewe na kwamba mwezi Disemba mwaka huu anakuja ili akamalishe taratibu za ndoa.
Lakini kinachonipa wasiwasi kwake ni suala la mawasiliano kwani naweza nikimpigia simu huwa anapokea kwa nadra sana na mara nyingi mpaka nianze mimi kumtafuta kwenye simu.
Je huyu mtu yuko serious kweli?
Nahitaji ushauri wenu tafadhali.