ushauri mzuri sana,:-DB-)......kila chupi itadondoka mbele ya hela
Sasa si umeshaambiwa kuwa ana mchumba? unataka amuache mchumba wake akufuate ww,wakt hata ww bado haujajua unataka nini katika mapenzi mwanzoni ulikuwa na wanawake hao wawili na moyo wako ulishindwa kufanya chaguo sahihi mwisho wa siku unawataka wote wawili maana huyu mwingne haujamuacha na mwingine unamfukuzia "mtaka yote kwa pupa hukosa yote"
Mimi ni kijana niliyehitimu masomo yangu ya chuo kikuu mwaka huu nina umri wa miaka 24, wakati nikiwa chuo nilibahatika kukutana na wasichana wawili wazuri sana ambao kwa nyakati tofauti niliweza kuwaeleza hisia zangu kwao. Niliwa bado chuon mmoja alinikubalia na tukaanza uhusiano ila baada ya muda nilihisi ananisaliti na nilifuatilia nikagundua kuwa ni kweli nilipomweleza aliniomba msamaha na kutokana na uzuri wake na namna nilivyokuwa nimemtambulisha kwa marafiki zangu sikuweza kumuacha nililazimika kendelea naye. Ila toka hiyo hali hiyo itokee hisia zangu kwake zilipungua sana na niliamua kumuacha ila alikuwa akilia sana na kunisisitiza kuwa nisimwache kutokana na roho ya huruma niliendelea kuwa naye ila sina hisia naye hata kidogo ingawa ni mzuri sana na anaonesha kunipenda sana.
Kwa upande wa huyu mwingine alipomaliza shahada yake ya kwanza alijiunga na masters na tuliendelea kuwa marafiki kama kawaida na tulifika hatua ya kuelezana hadi baadhi ya siri zetu, na huwa aliyokea kuniamini sana, kama ilivyokawaida nilijaribu kujieleza hisia nilizonazo kwake na alinikatalia kwa kigezo kuwa yupo na mchumba wake, sikuchoka kumsisitiza ila kinachoniumiza ni kuwa nampenda sana huyu dada wa pili ila nikimtumia SMS huwa hajibu nikimpigia simu akipokea huwa haongei sana, nimejaribu kutumia kila njia nimeahindwa ila nampenda sana, naombeni wana jf nifanye nini jamani nakosa raha kabisa. Huyu niliyemtongoza na akanikubalia yeye ananipenda sana ila mimi sina hisia kwake, but huyu wa pili anayesoma masters yeye kwa miaka mitatu yote niliyokuwa nilimtongoza ananikatalia ila nampenda sana na huwa nakosa raha kwa kuwaza namna ya kumpata. Naomba mnisaidie plz.
Komaa nae,usimuache huyo unaedai anakupenda na usiache kuendelea kumtongoza huyo wa masters,miaka 3 mbona michache sana,watu tunatongoza had miaka 8 ila mwisho wa siku tunafanikisha,endelea kuchapa wengne huku unakumbushia upande wa pili,usiache kukumbushia,ikiwezekana daily.
Nitakuwa tofauti kidogo na matazamio ila nahisi naweza saidia. Ndugu kuna mambo mengine tunaweka positive outcimes tunapoyafanya, mf unapoingia chuo unawaza kumaliza salama, hua hatuwazii sup,repeat au disco ingawa zipo, sasa ktk mambo ya mapenzi kuna kukubaliwa na kukataliwa yote lazima uyatreat kama expected outcomes, mtu ana mchumba! Then we unamtaka! Sasa unataka aachane na mchumba wake awe na wewe au! Ktk maelezo yako umesema huyo wa awali ulimpenda ila ulivyogundua anakusaliti upendo ukapoa! Sasa huyu unaemtaka ambae ana mchumba nae ukigundua hajaachana na mpenzi wake upendo wako utabaki levo hiyo hiyo, utaongezeka au utaoungua! Pili ukitaka kufanya maamuzi jifunze pia kujiweka ktk nafasi ya mwingine, je wewe ungekuwa ndio mchumba wa huyo dada suala hilo kwako lingekufurahisha! Ungetamani uachwe! Na mara nyingi what goes around comes around! So ukitaka the best then make sure u give the best! Jifunze kusamehe,kama huyo dada huwezi kuwa nae kwakuwa haukumpenda bali ulimtamani basi subiri utampata wa kufanana nawe badala ya kupenda wachumba wa watu,omba Mungu na muombee mwenzako,level ya uchumba ni hatua kuelekea ktk ndoa,don't mess na furaha ya wenzako. Wanawake ni wengi sana kitakwimu kuliko wanaume,utampata wa kwako. Sindano hua inauma ila ndio tunapona,ninaweza nikawa nimeongea njee ya matazamio ila ninaamini ni kwa ajiri ya kukujenga zaidi. Karibu tena
Like siioni hapa.Nitakuwa tofauti kidogo na matazamio ila nahisi naweza saidia. Ndugu kuna mambo mengine tunaweka positive outcimes tunapoyafanya, mf unapoingia chuo unawaza kumaliza salama, hua hatuwazii sup,repeat au disco ingawa zipo, sasa ktk mambo ya mapenzi kuna kukubaliwa na kukataliwa yote lazima uyatreat kama expected outcomes, mtu ana mchumba! Then we unamtaka! Sasa unataka aachane na mchumba wake awe na wewe au! Ktk maelezo yako umesema huyo wa awali ulimpenda ila ulivyogundua anakusaliti upendo ukapoa! Sasa huyu unaemtaka ambae ana mchumba nae ukigundua hajaachana na mpenzi wake upendo wako utabaki levo hiyo hiyo, utaongezeka au utaoungua! Pili ukitaka kufanya maamuzi jifunze pia kujiweka ktk nafasi ya mwingine, je wewe ungekuwa ndio mchumba wa huyo dada suala hilo kwako lingekufurahisha! Ungetamani uachwe! Na mara nyingi what goes around comes around! So ukitaka the best then make sure u give the best! Jifunze kusamehe,kama huyo dada huwezi kuwa nae kwakuwa haukumpenda bali ulimtamani basi subiri utampata wa kufanana nawe badala ya kupenda wachumba wa watu,omba Mungu na muombee mwenzako,level ya uchumba ni hatua kuelekea ktk ndoa,don't mess na furaha ya wenzako. Wanawake ni wengi sana kitakwimu kuliko wanaume,utampata wa kwako. Sindano hua inauma ila ndio tunapona,ninaweza nikawa nimeongea njee ya matazamio ila ninaamini ni kwa ajiri ya kukujenga zaidi. Karibu tena