Naomba ushauri

Naomba ushauri

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Posts
5,958
Reaction score
2,965
Ma GT habari zenu.Ninaomba ushauri kwa niaba ya rafiki yangu.Ameolewa kwa maana ya ndoa.Maisha ni mazuri kiasi.Tatizo Mume wake hataki kumtambulisha kwa ndugu zake wa tumbo moja,wala kwa mama yake mzazi.Ndoa yao ina miaka 12 na pia hatak kumpeleka mkewe kwao alipozaliwa.Siku ya ndoa yao jamaa aliwaalika ndugu ambao ni binam zake tu.Mke alijua kuwa hao ndo ndugu kumbe si hao bali wapo ndg wa tumbo 1 ambao jamaa hataki kabisa mkewe awajue.Je nimshauri nini rafik kwa maelezo hayo?
 
Mshauri atafute bwana mwingine. Lakini kumbuka muda wake upita.
 
du! ndo suluhisho? Huyo bwana mwingine ataisidiaje kuhusu hili. fafanua mkulu Kiba
 
mmmh nyumba ndooogo huwa inatambulishwa kweli
 
Hii habari ina chembechembe za kutungwa...miaka 12 unaifahamu au unaisikia...kwa kifupi tu miaka 12 naweza kuimithilisha na muda ambao mtoto anaanza darasa la kwanza hadi kidato cha nne
 
Si amuulize mumewe, huenda anamuepusha na ndugu zake.
 
Ikiwa habari hii ni ya kweli Aende akawaulize hao binamu zake na mumewe mbona simple tu. Afanye jambo hilo kwa siri . Na kumbuka penye nia pana njia
 
Mmh design ka ya uongo
Ila kama n kweli kajitakia tu kutowajua
Ndoa ilifungwa kidin au kiserkali?
Dini ipi?
Hao binam kashawah waulza kuhusu hao wazaz?
au ailjuaje kama ana wazaz?
Wana watoto?
Huyo "mume" anasemaje kuhusu hao wazaz wake?
 
Walioanaje hao? Au hawajafunga ndoa wamesogwzana?
Ina maana ndugu hawakuja harusini??
 
Back
Top Bottom