Nilikuwa na msichana
mmoja niliunganishiwa na dada yake na huyo msichana,sasa siku ya kwanza
kukutana siu ileile yule msichana akaniuliza nimevutiwa na yeye ama
hapana mimi nikakubari nimevutiwa nae,ni kweli alikua na vitu baadhi
navikubali kwake,siku mbili baada ya kuonana nikaandikiwa na yule dem
akidai TUACHANE akiwa na visingizio eti yeye akikosa vocha ya kunitumia
sms anaumia sana wakati time zingine nilikua nina mtumia vocha,sababu
nyingine anadai nimwache na yeye asogee level ya chuo kama mimi wakati
huo yupo 4m five mimi nipo diploma,ilo swala tukasuluhisha likaisha mara
ya pili tena nikatumiwa sms TUACHANE kwa vigezo vya ajabu ajabu,mara ya
tatu tena tukashindana kwa kitu kingine coz yule dem ni mbishi
balaa,aliniazimisha kitu chake alipokihitaji akatuma mtu akifate,mimi
hapo hapo nikaona huu ni upuuzi japokua dada yake tunaheshimiana sana
nikaamua kumpiga chini yule dem,siku ile le akanywa vidonge ajiue bahati
nzuri nikampigia sim mfanyakazi wao simu kumjulisha so alipozidiwa
akaenda kuwashitua wakubwa wakampatia maziwa akapona,sasa hivi
tunawasiliana kimagumashi sana mimi ndo niliamua kupunguza mawasiliano
sana,lakini ata hivyo huyu dem hashituki saaana,ila siku akituma sms
anaonekana kama mtu ambae bado hajanikatia tamaa,na dada yake bado
sijamweleza mpango wa kumwacha mdogo wake,nisaidieni hapo wadau