Nashukuru sana wote kwa ushauri wenu, ila mimi wasiwasi wangu ni kuwa je ni kweli anamaanisha anachokisema?
Maana kwa jinsi ninavyomuelewa anaweza kusema hivyo lakini bado hajawa na maamuzi kamili. Na wasiwasi wangu umenidhihirishia baada ya sasa kuanza vituko,
Mfano jumamosi nilimuuliza kama ataenda na watoto kumuona babu yao anaeumwa akasema hajajua, baada ya mimi kuondoka kwenda kazini alikwenda nao na akawaacha walale huko bila kunitaarifu, na hapo yule mtoto wa kwetu wote naumwa na kuna dawa anatumia na ameziacha nyumbani, baada ya mimi kurudi nyumbani na kugundua kuwa mtoto hatarudi na dawa ameziacha nikampigia kumuuliza sasa tunafanyaje maana dose itaharibika, akasema subiri nakuja tena kwa hasira, na aliporudi alikuwa kimya wala hakulizungumzia na likuwa amelewa, asubuhi pia akawa kimya, sasa ni visa tu na juzi amempeleka mtoto kwa aunt yake bila mimi kujua pia mpaka leo hajarudi, yaani kama mtu mwenye bifu fulani hivi na maelewano hakuna, na jana amelala kwenye chumba cha watoto.
Hio ndioo hali halisi ndugu zangu haya naendelea kusikiliza ushauri wenu.
Mpendwa nimecheka kweli asubuhi ya leo eti sijui ataniconvisi vipi nikapime. Kama anavyosema dena jamani kupima kwataka moyo lol, na sio rahisi mume ajue we unao ye hana akubali kirahisi rahisi hivyo, hawa wenzetu akikufumania tu ni kasheshe haya asikie umeukwaa huko si balaa.
Dena kama ndio wapimaga watu nyie watu wa ushauri nasaha mnajua kututisha, Mi nikienda kupima nawaambiaga naomba msinipe ushauri nasaha nipimeni na nipeni tu majibu. pengine umekutwa positive lakini mshauri ataanza bwana ooh unajua ukimwi this, ukimwi that mpaka jasho linakuchuruzika akimaliza ndio anakwambia hongera uko positive kha! hapo moyo karibu uachane na mwili.
Dnt take me worng but i nid to know wewe ulipata wapi hiyo ugonjwa? Nikijua hiyo naweza nikakushauri!
Ahasante (Pihu)
Mimi kama sijapata kwake basi nitakuwa nilipata kabla ya kuolewa
Huo ndio ukweli wangu ndugu yangu.
mmh..inawezekana hii?? kwa ufahamu wangu naona kama mwanaume akiathirika mwanamke pia anakuwa kwenye hatari kubwa ya kuathirika..
Ila kwa tukio la huyu dada yetu mpendwa ni kwamba yeye ameathirika lakini mumewe hajaathirika,.. ndo nilikuwa nataka kujua kumetokea nini??
Any way, vyanzo viko vingi, na cha msingi ni kusahau yaliyotokea na kuendelea na maisha..
Ahasante (Pihu)
Mimi kama sijapata kwake basi nitakuwa nilipata kabla ya kuolewa
Huo ndio ukweli wangu ndugu yangu.
Huyo mumeo ni muongo sana tena wa kutupwa..........................iko siku utakuja kusema hapa.................wanaume walivyo wakali eti akubali hali uliyonayo ha ha ha ha ha wewe unacheza na kusikia kwenye redio akubali eti yeye mzima sio kweli nikwambie..........................
Ahasante (Pihu)
Mimi kama sijapata kwake basi nitakuwa nilipata kabla ya kuolewa
Huo ndio ukweli wangu ndugu yangu.
Umesema upo kwenye ndoa kwa miaka 13, ila kwa miaka 3 ya hivi karibuni hali yako imezidi kuzorota..
Nilitaka kufahamu ni nani aliyekuambikiza?..Maana kama mume amesema kapima na hajaonekana nao, ninapata wasiwasi na uaminifu kwenye ndoa.
Hilo ndo nililosema mimi huyo mumeo huyo shika mkono nenda nae mkapime wote uone matokeo....................kiukweli mimi kwa uzoefu wangu simuamini kabisa
Too general DA, wa2 wa namna hiyo wapo na huko CTC anako chukua dawa huyo dada huduma ya ushauri wa namna ya kuishi wenza wenye HIV status walonazo ipo, hivo wai2mie, kizuri zaidi ni kuwa hata mwenzie kaacha kujinyanyapaa amini wakizingatia wataish maisha ya amani!.KUNA IMPROVEMENT KUBWA MNO KTK HIV MANAGEMENT TOFAUTI NA HAPO AWALI SEMA TU JAMII NDO HAIJAELIMIKA VYA KUTOSHA NDO MAANA INAKUWA NGUMU KU2MIA HIZO HUDUMA ZILIZO TAYARI. Kwakifupi waende wote ctc kuna msaada mkubwa tu.Huyo mumeo ni muongo sana tena wa kutupwa..........................iko siku utakuja kusema hapa.................wanaume walivyo wakali eti akubali hali uliyonayo ha ha ha ha ha wewe unacheza na kusikia kwenye redio akubali eti yeye mzima sio kweli nikwambie..........................
Historia hiyo Haitasaidia chochote hapo,.....wote wawili waende kwa mnasihi mwenye taaluma ambao wengi hupatikana ctc na huduma hiyo haina malipoDnt take me worng but i nid to know wewe ulipata wapi hiyo ugonjwa? Nikijua hiyo naweza nikakushauri!
Dada, kwanza mm nakukaribisha sn ktk mtandao wetu wa sema usikike ktk jamii yetu, ila usivunje sheri, kwa mtu yeyote aliyeko humu kwenye mtandao au nje ya mtandao kwa kudhalilisha kwa namn yoyote ile, ili uwanja na carpet let au jamvi letu liweze kuwahabarish maelfu ya watu,Habari wana jamii wote,ni mara yangu ya kwanza kuingia huku kwenye forum hii
Naomba sana mnipe ushauri wenu kwa haya nitakayoyaeleza hapa
Mimi nimeolewa nina miaka 13 katika ndoa, nina mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 12, mume wangu ana mtoto wa kike mwenye miaka 10 aliezaa na mwanamke mwingine.
tatizo langu ni kuwa miaka mitatu iliyopita niligundua kuwa nimeathirika na sasa natumia dawa za kupunguza makali(ARV)
Nilishindwa kumweleza mume wangu kuhusu hali yangu kwa kuwa kila nilipomshauri kuhusu kupima afya alikuwa hataki akidai kuwa siku akigundua kuwa ameathirika atakufa. Ila mimi nilipogundua kuwa nimeathirika nikawa sikubali kufanya mapenzi bila kutumia kinga, ingawa wakati mwingine alikuwa analazimisha lakini sikuwa tayari.
Hivi karibuni akanieleza kuwa amegundua kuhusu hali yangu baada ya kuona kadi yangu ya clinic, na yeye ameenda kupima na amesema yeye hajaathirika, hivyo kasema tuendelee kuishi bila watu kujua.
Mimi nikampa option kuwa kwa kuwa yeye ni mzima basi nisimbane kama atahitaji awe na mwenza mwingine basi tunaweza kuachana na yeye akaanza maisha mapya, lakini kasema kuwa haiwezekani tuachane kwa kuwa tumeishi muda mrefu na tumesaidiana mengi.
sasa naomba ushauri wenu je hili linawezekana? Au mna ushauri gani?
Ahasanteni
Mhhh! DA wapo wenye mioyo kama ya huyu bwana (kama ni kweli yuko negative) ingawaje ni wachache sana, ila kwa waume/wake wengi uamuzi kama huu ni mgumu sana unapogundua mwenzio ameathirika na wewe mambo yako bado yako safi. Pamoja na kujua kwamba hupati maambukizo kwa kushare nyumba, kitanda, vyombo n.k. lakini mhhhhh! inahitaji moyo sana.