Naomba ushauri wenu: Nataka nijenge chumba kimoja

Hongera kwa kufikiria hilo, utakuwa umefanya jambo muhimu mno. Ila hao mafundi walevi angalia nyumba yako isije kuwa ya kilevi.
emoji16.png
huko singida kuna mawe ya kujengea msingi au huwa mnatumia tofali?
Kabisa hapo kwa mafundi walevi achunge sana
Wakuu wenye uzoefu na maisha shikamooni.

Mimi nafanyabiashara ambayo inaniingizia 7000 kwa siku kama faida

Sasa nina kiwanja heka moja mother aliniachia kimekaa muda mrefu hakina Kazi kilikuwa kikitumika Kama shamba nako hakitoi mazao mengi kwasababu eneo Lina kichuguu

Sasa Mimi nataka kujenga angalau master room moja ambayo Ina choo ndani na kasebule, maana nafikiria huku kupanga kila mwezi nampa mwenye nyumba 30000 nimeona Bora nijenge nishaurini nitumie mbinu gani kufanikisha gharama yake maana nawaza niwe nanunua mifuko ya cement mitano kila week naiweka au nifanyeje?

Na je nahitaji ramani kwenye kanyumba Kama hako? Kuhusu msingi gharama zake zipoje?

Cha kufurahisha kuna mafundi flani ni walevi sana Bei zao nimesikia ni nzuri nawaza niwatumie wao au niwatumie tu Mafundi wazuri, lakini nataka finishing iwe nzuri decorations ziwepo yaani sebuleni niweke wallpaper na tv cabinet japo nitaweka solar maana nitakuwa nalala tu asubuhi naenda kwenye kibarua changu.

Nishaurini nianzie wapi kuhusu mchanga hakuna shida huku singida mchanga upo wa kutosha.

Nijiandae vipi niweke hela mpaka ifike milioni kadhaa au nijenge tu kwa plan hio mdogomdogo?
Hapo kwa mafundi walevi acha a nao
 
Kwenye ujenzi nakushauri ujenge kitu simple ila kiwe kizuri, hao mafundi walevi achana nao. Jenga kajumba kadogo chenye ramani nzuri sana haswa upande wa madirisha yawe makubwa hewa ya kutosha na pia paa liwe juu sio nyumba ndogo halafu fupi.

We anza msingi ukimaliza nyanyua boma ukimaliza piga bati nenda steji kwa steji usinunue mabati wakati hata msingi bado
 
Wakuu wenye uzoefu na maisha shikamooni.

Mimi nafanyabiashara ambayo inaniingizia 7000 kwa siku kama faida

Sasa nina kiwanja heka moja mother aliniachia kimekaa muda mrefu hakina Kazi kilikuwa kikitumika Kama shamba nako hakitoi mazao mengi kwasababu eneo Lina kichuguu

Sasa Mimi nataka kujenga angalau master room moja ambayo Ina choo ndani na kasebule, maana nafikiria huku kupanga kila mwezi nampa mwenye nyumba 30000 nimeona Bora nijenge nishaurini nitumie mbinu gani kufanikisha gharama yake maana nawaza niwe nanunua mifuko ya cement mitano kila week naiweka au nifanyeje?

Na je nahitaji ramani kwenye kanyumba Kama hako? Kuhusu msingi gharama zake zipoje?

Cha kufurahisha kuna mafundi flani ni walevi sana Bei zao nimesikia ni nzuri nawaza niwatumie wao au niwatumie tu Mafundi wazuri, lakini nataka finishing iwe nzuri decorations ziwepo yaani sebuleni niweke wallpaper na tv cabinet japo nitaweka solar maana nitakuwa nalala tu asubuhi naenda kwenye kibarua changu.

Nishaurini nianzie wapi kuhusu mchanga hakuna shida huku singida mchanga upo wa kutosha.

Nijiandae vipi niweke hela mpaka ifike milioni kadhaa au nijenge tu kwa plan hio mdogomdogo?
Jenga mdogo mdogo. Nashindwa kuapload picha ninge kutumia karamani ka self ya room 1 nzuri
 
Cement usinunue Sasa inaweza ganda ukaingia hasara

Anza nunua bati na mbao

Kisha nunua tofali hasa zile za mwendokasi utaokoa Sana utapunguza gharama za ujenzi kiasi chake .

Nunua mchanga kabisa.

Nunua tiles na madirisha na mlango kabisa

Kisha ndio ununue simenti.

Mtafute fundi ikiwezekana uwe una mpiga tafu kuipandisha mdogo mdogo kuokoa gharama za vibarua .

Fasta tu utahamia kwako
Hata mbao asinunue zitapinda
 
Back
Top Bottom