Naomba ushauri: Nimepata fursa ya kwenda USA kusoma

Plan Of Action

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
462
381
Habari za Jumapili mabibi na mabwana?

Katika harakati zangu za kusaka scholarships za kusoma Degree ya Pili katika fani za uongozi, nimekutana na hii ya kwenda USA lakini kusoma Masters ya dini chuo kimoja huko Michigan.

Nimeambiwa masomo hayo yanafadhiliwa 100% na kanisa na ni mwendo wa miaka minne!

Dah, mpaka sasa nimeshindwa kukataa wala kukubali, wamenipa muda nijifikirie kabla hawajampa fursa mtu mwingine!

Naombeni ushauri wana Jamvi, nina Degree ya kwanza ya Logistics. Je, niende US nikasome Divinity?

Je, nitakutana na fursa gani mbeleni baada ya kuhitimu? Maana sikuwa na mawazo yoyote kuhusiana na dini.

Karibuni kwa ushauri!
 
Habari za Jumapili mabibi na mabwana?

Katika harakati zangu za kusaka scholarships za kusoma Degree ya Pili katika fani za uongozi, nimekutana na hii ya kwenda USA lakini kusoma Masters ya dini chuo kimoja huko Michigan.

Nimeambiwa masomo hayo yanafadhiliwa 100% na kanisa na ni mwendo wa miaka minne!

Dah, mpaka sasa nimeshindwa kukataa wala kukubali, wamenipa muda nijifikirie kabla hawajampa fursa mtu mwingine!

Naombeni ushauri wana Jamvi, nina Degree ya kwanza ya Logistics. Je, niende US nikasome Divinity?

Je, ntakutana na fursa gani mbeleni baada ya kuhitimu? maana sikuwa na mawazo yoyote kuhusiana na dini.

Karibuni kwa ushauri!
Nipe mimi fulsa hiyo
 
Kama huna interest hiyo ya kusoma divinity ,achana nayo kabisa. Haya mambo ya dini watu wanayafanya kibiashara lakini anastahili kua kiroho zaidi.The willingness to serve ,that special call to be an evangelist lakini si eti umeambiwa uende marekani kisa unaenda kusoma divinity then unaenda. Piga chini tafuta alternative nyingine.Usilazimishe
 
Mkuu kama hutojali, ni chuo gani hicho? Unaposema wanaomba $50 kwa ajili ya application inamaanisha hata application hujatuma au? Ni vigumu sana kupata scholarship ya maneno USA. Unatuma kwanza applications zinapitiwa ndio wanasema kama umepata scholarship or not. Naongea from experience. Swala la degeree sio inshu, unafika unazuga nayo kama muhula mmoja halafu unabadilisha. Hii mbinu wanaitumia sana watu wa Asia kuingia top university, anaapply coz simple tu anakuwa amekubali kuharibu semester baadaye anabadilisha.
 
Angalia usije ukaingizwa mjini wewe. Unaweza kukuta ni wajanja wa mjini wanataka wakupige. Hutaamini we ingia kichwa kichwa uone

Ndio hata mimi nimemwambia mkuu, haiwezekani ukapewa scholarship ya maneno USA. Unapata scholarship kabla ya kulipia ada ya application, vigumu kumeza
 
Yaani wewe bro una digrii ya kwanza ya logistiks lakini bado unashindwa kufanya uamzi kama uende kusoma masters ya divinity au la! kweli?

Unasema ulikuwa unatafuta chuo usome masters ya uongozi lakini ukakutana na ofa ya kusoma mambo ya dini huko USA umechanganyikiwa, naona unaingizwa mkenge huku unaona.

Elewa habari ya dini si kitu cha mchezo lazima uwe na wito, huwezi kuchukuliwa kienyeji bila kufanya application from nowhere ukapelekwa kusoma mambo ya dini Marekani unless unapelekwa chuo cha mafreemason huko Michigan ambako inasemekana ndiko kuliko na makanisa maarufu ya Freemason.
Chunga sana bro.
 
Mkuu kama hutojali, ni chuo gani hicho? Unaposema wanaomba $50 kwa ajili ya application inamaanisha hata application hujatuma au? Ni vigumu sana kupata scholarship ya maneno USA. Unatuma kwanza applications zinapitiwa ndio wanasema kama umepata scholarship or not. Naongea from experience. Swala la degeree sio inshu, unafika unazuga nayo kama muhula mmoja halafu unabadilisha. Hii mbinu wanaitumia sana watu wa Asia kuingia top university, anaapply coz simple tu anakuwa amekubali kuharibu semester baadaye anabadilisha.
kaka asante kwa ushauri. Hio usd 50 inalipwa baada ya kutuma application, wanakupa namna ya kulipa kisha ndipo wanaanza kuiprocess hio application..

sijui kama nimeeleweka hapo!
mimi binafsi alienipa hio dili aliniambia same thing, kuwa kama nikisoma mwaka mmoja naweza badili kwenda course nyingine niipendayo. Chuo kiko michigan, kabla application haijakubaliwa wanataka 50$ kwanza, dah hapo nimeishiwa pose.

Halafu bado nauli ya ndege unajilipia mwenyewe eti ukifika huko ndio wanakurudishia, ndivyo huyu aliniambia!!

Yani imenibidi nimpigie simu leo nimemwambia siwezi.

Dili ikaishia hapo!
 
Yaani wewe bro una digrii ya kwanza ya logistiks lakini bado unashindwa kufanya uamzi kama uende kusoma masters ya divinity au la! kweli?

Unasema ulikuwa unatafuta chuo usome masters ya uongozi lakini ukakutana na ofa ya kusoma mambo ya dini huko USA umechanganyikiwa, naona unaingizwa mkenge huku unaona.

Elewa habari ya dini si kitu cha mchezo lazima uwe na wito, huwezi kuchukuliwa kienyeji bila kufanya application from nowhere ukapelekwa kusoma mambo ya dini Marekani unless unapelekwa chuo cha mafreemason huko Michigan ambako inasemekana ndiko kuliko na makanisa maarufu ya Freemason.
Chunga sana bro.
Asante sana kaka, maamuzi sio kwamba nimeshindwa kufanya, la hasha!

Ishu hapa ni kwamba, natafuta ushauri, maana kwa mujibu wa mwenyeji wangu anasema nitakuwa na uwezo wa kubadili mwelekeo wa elimu baada ya mwaka mmoja, yani nisome kila ninachokilenga!

Sikutaka kumkatalia moja kwa moja ila nimemwambia nitampa majibu baada ya upembuzi yakinifu...

Mkuu ndio maana natafuta ushauri kwa wajuvi, kuwa na degree sio kujiamulia mambo mwenyewe
 
Unaweza kuwa unasoma masters ya Divinity huku unapiga Open master ya kitu kingine kwa miezi 18, acha ushamba nenda usichezee bahati.
 
Asante sana kaka, maamuzi sio kwamba nimeshindwa kufanya, la hasha!

Ishu hapa ni kwamba, natafuta ushauri, maana kwa mujibu wa mwenyeji wangu anasema nitakuwa na uwezo wa kubadili mwelekeo wa elimu baada ya mwaka mmoja, yani nisome kila ninachokilenga!

Sikutaka kumkatalia moja kwa moja ila nimemwambia nitampa majibu baada ya upembuzi yakinifu...

Mkuu ndio maana natafuta ushauri kwa wajuvi, kuwa na degree sio kujiamulia mambo mwenyewe
Wasiliana na balozi wa Tanzania aliyeko Marekani kupata information za hicho chuo, mambo ya Freemason ni mambo ya kizamani sana.
 
Umesoma logistics halafu unataka kuichezea,nadhani sa hz ulitakiwa uwe unawazia Erasmus University or MIT kama uko serious lakini
 
Back
Top Bottom