Nataka kujiajiri lakin sijui pakuanzia..Ninakipaji cha kutunga HADITHI za MOVIE na MASHAIRI kazi hii nimeanza tangu 2006,nilishawahi kufanya kazi na magazeti ya NIPASHE,MAJIRA na MWANANCHI baadhi ya HADITHI zangu ni HARUFU YA MAUTI,MTEJA ZUMBUKUKU,VUVUZELA,NILIMUUA MAMA,MALAIKA MWENYE MAPEMBE,USIPONIOA NITAKUROGA na nyingine kibao,pia huwa natunga mashairi ktk sherehe mbalimbali kama kipaimara,birthday,ndoa etc..nilifanya jitihada ili niweze kusimama mwenyewe ktk kazi hizo mfano mwaka 2012 nilimtafuta Shigongo nikapigwa za mbavu,nilitafuta waigizaji wa Bongo movie ili niwauzie story nikaambulia mateke kwa sababu eti mim sio maarufu kama wao..pesa ninazolipwa magazetin haziwez kunifikisha popote...je unanishauri nifanye nin ili niweze kuona matunda ya kipaji changu?Ahsanteni.