Naitwa Ahmady niko Dsm, mwaka jana nikiwa field nilitokea kumpenda msichana ambae nae alionesha dhahiri kwamba ana mapenzi ya dhati kwangu kwani vitu vingi alinifanyia kwa muda mchache ambao nilikuwa nae.
Ila mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambae tupo yapata miaka miwili tena mtoto nimezaa nae but muda umefika wa kuchagua mke wa kuoa naomba mnishauri wapi niende kati yao ?
Unataka tukuchagulie ili akikusumbua uje kulialia hapa JF , haya mkuu mi nakushauri tafuta wengine wawili kwanza tukuchagulie vizuri, multiple choice ya a na b hainogi, wajaze kuwe na a , b , c , d
huyo msichana uliekutana nae field, huenda ana mtu anaempenda sana kuliko wewe, na wameshawekeana hata ahadi ya kuoana, na huenda kashamzalia mtoto, ila yote hayo huwezi ukayajua. ila amekutana na wewe tu huko field kwa muda mfupi kama ajali..
Jiulize kwanini unasita kumuoa moja kwa moja na kumuacha mpenzi wako aliyekuzalia hadi mtoto, na ni kipi kilichokusukuma hadi uje na uzi wa kuomba ushauri!