Naomba ushauri, mpenzi wangu hana hamu na mimi hata kidogo

talk2me

Member
Jan 22, 2010
11
8
Habari,

Mimi ni kijana wa miaka 32 sasa. Ninae mpenzi wangu wa muda tangu 2009 wakati anasoma A level. Nimekua nae mpaka anahitimu chuo kikuu na Mungu ametujalia mtoto wa kike ana umri wa miezi 18 sasa. Tupo katika mpango wa kufunga ndoa mwaka huu na taratibu za awali zote nilishakamilisha (posa na mahari)

Cha kushangaza mpenzi wangu hana hamu na mimi hata kidogo japokua anaishi kwao nami kwangu lakini hata nikimuomba muda siku za weekends anakua na visingizio lukuki. I don't feel loved at all. Mimi ndiye nimekua nikipiga simu na kumjulia hali sababu yupo na mtoto. Siku nikinyamaza kimya basi hashtuki wala haoni shida anakaa kimya and bad enough huwa namuona online whatsapp.

Anafanya kazi na mahitaji ya mtoto natimiza kama Mzazi lakini sijui nini kimetokea hapa katikati amebadilika sana. Sijui hata where do I stand Kwakweli. Nikimuwaza anasema hamna kitu amechoka tu. Naombeni ushauri. Nifanyaje.
 
Pole sana mkuu, je hiyo tabia ya kuku-ignore ilianza tu baada ya kujifungua? maana nasema hivi sababu nami mke wangu wakati amejifungua niliona kabisa jinsi alivopoteza concentration sababu ya kuwa busy na mtoto. So usikute yuko busy na mtoto lakini sasa "not to that extent". Ongea naye ujue tatizo nini.
 
Habari!
Mimi ni kijana wa miaka 32 sasa. Ninae mpenzi wangu wa muda tangu 2009 wakati anasoma A level. Nimekua nae mpaka anahitimu chuo kikuu na Mungu ametujalia mtoto wa kike ana umri wa miezi 18 sasa. Tupo katika mpango wa kufunga ndoa mwaka huu na taratibu za awali zote nilishakamilisha (posa na mahari)

Cha kushangaza mpenzi wangu hana hamu na mimi hata kidogo japokua anaishi kwao nami kwangu lakini hata nikimuomba muda siku za weekends anakua na visingizio lukuki. I don't feel loved at all. Mimi ndiye nimekua nikipiga simu na kumjulia hali sababu yupo na mtoto. Siku nikinyamaza kimya basi hashtuki wala haoni shida anakaa Kimya and bad enough huwa namuona online whatsapp. Anafanya kazi na mahitaji ya mtoto natimiza kama Mzazi lakini sijui nini kimetokea hapa katikati amebadilika sana. Sijui hata where do I stand Kwakweli. Nikimuwaza anasema hamna kitu amechoka tu. Naombeni ushauri. Nifanyaje.
 
Attachments

  • FB_IMG_1492275543549.jpg
    FB_IMG_1492275543549.jpg
    22.6 KB · Views: 67
Kaa nae kitako uongee nae vizur mfungue akili kuwa sasa nyie ni mke na mume kupitia mtoto mlie nae...

Muweke wazi juu ya kitu mnachoenda kufanya yan ndoa ....

Akikuelew sawa asipojirekebisha utaingiza shetani ndani ya nyumba utsjuta maisha yako yote Dunia utaiona chungu kwako
 
Mmmmmh haya mahusiano bhana..... Any way. Pole mkuu ila ongea nae tu. ujue majaribu yapo sana hasa kwenye eneo LA ndoa. Usikate tamaa pengine ubize wa mtoto
 
Pole sana mkuu, je hiyo tabia ya kuku-ignore ilianza tu baada ya kujifungua? maana nasema hivi sababu nami mke wangu wakati amejifungua niliona kabisa jinsi alivopoteza concentration sababu ya kuwa busy na mtoto. So usikute yuko busy na mtoto lakini sasa "not to that extent". Ongea naye ujue tatizo nini.
Ni kweli alianza kuni'ignore baada ya mtoto kuzaliwa lakini nikajaribu kumuelewa but this time naona inavuka mipaka nimejaribu kuongea nae kama kuna kitu chochote au kama amepata mtu mwingine anakataa kua hana.
 
Hawa ni viumbe wa ajabu sana ishi nao kwa akili inawezekana ni maisha tu mpe mda fanya kama umemsahau mapenz cku zote as time go yanapungua
 
Habari!
Mimi ni kijana wa miaka 32 sasa. Ninae mpenzi wangu wa muda tangu 2009 wakati anasoma A level. Nimekua nae mpaka anahitimu chuo kikuu na Mungu ametujalia mtoto wa kike ana umri wa miezi 18 sasa. Tupo katika mpango wa kufunga ndoa mwaka huu na taratibu za awali zote nilishakamilisha (posa na mahari)

Cha kushangaza mpenzi wangu hana hamu na mimi hata kidogo japokua anaishi kwao nami kwangu lakini hata nikimuomba muda siku za weekends anakua na visingizio lukuki. I don't feel loved at all. Mimi ndiye nimekua nikipiga simu na kumjulia hali sababu yupo na mtoto. Siku nikinyamaza kimya basi hashtuki wala haoni shida anakaa Kimya and bad enough huwa namuona online whatsapp. Anafanya kazi na mahitaji ya mtoto natimiza kama Mzazi lakini sijui nini kimetokea hapa katikati amebadilika sana. Sijui hata where do I stand Kwakweli. Nikimuwaza anasema hamna kitu amechoka tu. Naombeni ushauri. Nifanyaje.

Kama haya maelezo uliyotueleza hapo juu ni ya kweli kabisa basi bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno au kutikisa masikio nakushauri tu upesi Mkuu nenda kaifuate Mahari yako au ipotezee kimoja na hizo taratibu zako / zenu za Ndoa ZISITISHE rasmi kwani hapo huna Mchumba na tayari ameshaanza kubanduliwa na hana tena Mapenzi ya kweli nawe.

Halafu ni mara chache sana couples za Shuleni au Vyuoni kuja kuwa za kweli na kufanikiwa na hata kama zipo zilizofanikiwa ni sisi tu huku nje tukiziona tunawaona wako vizuri lakini kiuhalisia hao wawili hawana upendo. Ila naona kwa wengi ambao wamekutana tu juu kwa juu hawa wakija kuamua Kuoana basi huishi vizuri mno.

Psychologically Mwanamke akikujua wakati bado wote mnasoma na bado hamna mwelekeo wenu mzuri wa Kimaisha hapo baadae hutengeneza dharau fulani hivi Kwako japo ukiwa nae atajitahidi kukuficha na mara nyingi huko huko Shuleni au Chuoni akitokea tu Mwanaume mwenye Kisu Kikali zaidi yako basi Mkuu utabanduliwa Mkeo hadi ujute kuifahamu dunia hii.

Siku hizi hakuna Mapenzi tena bali kuna drama tupu na tunadanganyana mno huku tukipana mgongo mafuta.
 
Ni kweli alianza kuni'ignore baada ya mtoto kuzaliwa lakini nikajaribu kumuelewa but this time naona inavuka mipaka nimejaribu kuongea nae kama kuna kitu chochote au kama amepata mtu mwingine anakataa kua hana.
Usichoke kuzungumza nae

Wakati mwingine wanawake hujali zaidi watoto.....
 
Mkaushie kwa wiki moja tu,huku ukiendelea kutuma hela ya matunzo,reaction yake itakupa mwanga juu ya msimamo eake
 
Back
Top Bottom