Hakuna Biashara Mbaya inategemea na Location yako na Mahitaji ya sehemu husika, sababu umeshajua margins ni kiasi gani basi kilichobaki ni wewe kujaribu kuona wateja sehemu ulipo wakoje na kazi ya mzigo kutoka. Mimi naweza kuuza ICE (Barafu) ni vigumu ila kumbe nipo kwa Eskimos wakati mtu aliyopo jangwa la sahara hii inaweza ikawa Hot Cake...
Kwa ushauri kama mtaji unao na unaona hizo margins sio mbaya tafuta hizi Paypoints (Selcom, Maxmalipo et al..) hapa hautasumbuka kuwa na stock ya vocha utakuwa unauza vocha ya aina yoyote na denomination yoyote mteja anayotaka..
Ila kwa ushauri wangu usinfanye hii kama biashara pekee bali biashara ya ziada wakati unauza na vitu vingine
Mkuu asante kwa ushauri mzuri, hii nimechukua kama shughuli ya ziada tu, ili niweze fikia malengo yangu. Samahani hizo paypoints, sijakupata vizuri unanishauri nikawuzie huko au nikaweke hapo vocha zangu, samahani nahisi sijakuelewa sawia ktk hili?
Niliposema hii iwe ni kitu cha ziada kuuza nilimaanisha kama ni kibanda usiuze vocha peke yake unaweza kuweka pipi, magazeti, na bidhaa nyingine...
Kuhusu paypoint kuna vile vifaa kama Selcom ambacho wewe unachofanya ni kujaza balance tu, na unaweza kuuza vocha zote na LUKU hii itakusaidia sana kama akija mtu wa kununua vocha ya elfu kumi, au mia mbili au elfu tano na wewe unazo za mia tano peke yake.., yaani mtu unampa vocha yoyote atakayotaka yenyewe inarushwa direct kwenye simu yake
Mungu akabariki kazi ya mikono yako kaka.
Hewala na ukafanikiwe.
Niliwahi kusikia kuwa voucher moja faida yake ni sh. 50 (stand to be corrected).
Kwa maana hiyo, endapo kwa siku ukauza voucher za mia tano mia tano 100 utapata faida ya sh. 5000 kwa siku ambayo ni sawa na sh. laki moja na nusu kwa mwezi.
Kwahyo itategemea zaidi malengo yako.
mdogomdogo ndio mwendo