Naomba tofauti kati ya kuwa Mpenzi na kuwa Mama kwa mwenza wako(mwanaume)

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
16,158
14,153
Kuna siku kulikua kuna uzi katikati kuna mdau akamjibu muanzisha uzi epuka kuwa mama wa mpenzi wako kuwa mwenza wake tu

Kiukweli haya mambo yanachanganya sana kwa maana kuna mambo ukiangalia mama yake alikua anamfanyia na uwenda wewe pia unamfanyia

Na kuna wanaume kiukweli wanadeka(wanahali flani) ya kupenda kufanyiwa mambo mengi sana ikiwemo kupewa maziwa jambo ambalo hata mama yake kalifanya
Anataka umueleze,umuandalie umpe muongozo kama mama yake jambo ambalo ni zuri
Kulingana na maelezo ya ile coment

Wanaume weng hawapendi mwanamke awe kama mama yake
Ugumu unakuja hapo namna ya kuwa na nafasi yako tu ya mpenzi/mke na sio mama ni kwa kufata yapi na
kuacha yapi?
Lakini swali la mwisho ni kweli hampendi mke/mpenzi kutenda kama mama yako juu yako?
 
Sure.......
Ila kwa ninavyojua na miaka yangu hii niliyokaa duniani wanaume wengi wanapenda tuwaleee kimama mpenzi ila tatizo na sisi sikuhizi hatupo huko, na yote yamesababishwa na wao kutothamini kile tuwapacho matokeo yake unyonge wetu umekuwa ndo fimbo ya kutuchapia, sasa matokeo yake wanawake nao wamekuwa mabindidu tu....
 
Mpendwa @masai dada wanaume wengi (ikiwemo mimi) huwa tunapenda kuwa cared kama watoto. Lakini jambo hilo linapaswa kuwa kiasi na mipaka. Kuna vitu ambavyo alivifanya mama yake mzazi ambavyo wewe mke hupaswi kuvifanya. Mfano: Mpendwa wangu @Heaven Sent amegusia kuhusu swala kumueleza mume/mpenzi wako pale anapokosea na ninaomba niwaeleweshe kitu hapa; Tatizo sio kumueleza mpenzi/mume wako kuwa amkosea, tatizo ni njia au namna ambayo unaitumia kumueleza huyo mpenzi/mume wako kuwa amekosea na yeye aweze kukuelewa na kukiri kuwa amekosea. Na hapa ndipo wengi wetu tunapokosea.

Mfano: Unakuta mpenzi/mumeo amerudi nyumbani usiku amachelewa, pengine inawezekana ikawa bahati mbaya labda alipatwa na tatizo au dharura ambayo imepelekea yeye kuchelewa kurudi nyumbani. Mke mnyenyekevu, mwenye hekima na busara atamkaribisha mumewe/mpenzi wake na kumpa chakula na maji ya kuoga ili apate kupumzika na kutafuta mda muafaka wa kumuuliza mpenzi/mume kwa nini amechelewa kwa upole na upendo. Muda huo muafaka utategemea pia na mood aliyonayo mume wako kwa wakati huo.

Lakini wengi huwa tunafanya tofauti, unakuta wengine wanakaribisha wapenzi wao kwa kufoka na kuwamalizia hasira zao zote na wengine huridiriki kujidai wao ni ma John Cena na kuanza kurusha makofi... Sasa kwa hali hiyo hata kama huyo mumeo au mpenzi wako amkosea unategemea atakuelewa?

Kumbuka huyo ni mpenzi/mumeo hivyo ni lazima umheshimu na umtreat kwa upendo na sio kumfokea, na kumjibu kadiri ya unavyojisikia hasa pale anapokosea. Kufoka kunaweza kufanywa na mama mzazi lakini sio wewe mke.
 
Ila kwa ninavyojua na miaka yangu hii niliyokaa duniani wanaume wengi wanapenda tuwaleee kimama mpenzi ila tatizo na sisi sikuhizi hatupo huko, na yote yamesababishwa na wao kutothamini kile tuwapacho matokeo yake unyonge wetu umekuwa ndo fimbo ya kutuchapia, sasa matokeo yake wanawake nao wamekuwa mabindidu tu....
Ni kweli kabisa.

Ni kama Man Utd walizoea kupetiwa mama mpenzi na FA, marefa na brown envelope.

Lakini mambo yamebadilika wanalia kama Watoto.

Samahani kama wewe ni shabiki wa Man U. If yes am so so sorry madam
 
@masai dada mimi sioni sababu ya kudeka kwa mwanamke issue in kila mtu ajue wajibu wake kwenye mahusiano tu. mambo ya ww kua mama utanidanganya tu
 
Ni kweli kabisa.

Ni kama Man Utd walizoea kupetiwa mama mpenzi na FA, marefa na brown envelope.

Lakini mambo yamebadilika wanalia kama Watoto.

Samahani kama wewe ni shabiki wa Man U. If yes am so so sorry madam
Hahahhahhha Wewe nichokoze tu tutakutana kule kule kwetu nikupe yako hapa nipo kimahusiano,kirafiki na kimapenzi zaidi.
 
Kuna siku kulikua kuna uzi katikati kuna mdau akamjibu muanzisha uzi epuka kuwa mama wa mpenzi wako kuwa mwenza wake tu

Kiukweli haya mambo yanachanganya sana kwa maana kuna mambo ukiangalia mama yake alikua anamfanyia na uwenda wewe pia unamfanyia

Na kuna wanaume kiukweli wanadeka(wanahali flani) ya kupenda kufanyiwa mambo mengi sana ikiwemo kupewa maziwa jambo ambalo hata mama yake kalifanya
Anataka umueleze,umuandalie umpe muongozo kama mama yake jambo ambalo ni zuri
Kulingana na maelezo ya ile coment

Wanaume weng hawapendi mwanamke awe kama mama yake
Ugumu unakuja hapo namna ya kuwa na nafasi yako tu ya mpenzi/mke na sio mama ni kwa kufata yapi na
kuacha yapi?
Lakini swali la mwisho ni kweli hampendi mke/mpenzi kutenda kama mama yako juu yako?
@masai@dada ulikuwa umeolewa nini maana muda tangu nikuone..
Ndoa vipi au imevunjika km UKAWA maana nilikuona mara ya mwisho tukimpambania Lowasa..!
 
Mpendwa @masai dada wanaume wengi (ikiwemo mimi) huwa tunapenda kuwa cared kama watoto. Lakini jambo hilo linapaswa kuwa kiasi na mipaka. Kuna vitu ambavyo alivifanya mama yake mzazi ambavyo wewe mke hupaswi kuvifanya. Mfano: Mpendwa wangu @Heaven Sent amegusia kuhusu swala kumueleza mume/mpenzi wako pale anapokosea na ninaomba niwaeleweshe kitu hapa, Tatizo sio kumueleza mpenzi/mume wako kuwa amkosea, tatizo ni njia au namna ambayo unaitumia kumueleza huyo mpenzi/mume wako kuwa amekosea na yeye aweze kukuelewa na kukiri kuwa amekosea. Na hapa ndipo wengi wetu tunapokosea.

Mfano: Unakuta mpenzi/mumeo amerudi nyumbani usiku amachelewa, pengine inawezekana ikawa bahati mbaya labda alipatwa na tatizo au dharura ambayo imepelekea yeye kuchelewa kurudi nyumbani. Sasa badala ya wewe mke kuwa mnyenyekevu na busara kwa kumkaribisha mumeo/mpenzi wako na kumpa chakula na maji ya kuoga ili apate kupumzika na kutafuta mda muafaka wa kumuuliza mpenzi/mume kwa nini amechelewa kwa upole na upendo na Muda huo muafaka utategemea pia na mood aliyonayo mume wako kwa wakati huo. Lakini wengi huwa tunafanya tofauti, unakuta wengine wanakaribisha wapenzi wao kwa kufoka na kuwamalizia hasira zao zote na wengine huridiriki kujidai wa ni ma John Cena na kuanza kurusha makofi, sasa kwa hali hiyo hata kama huyo mumeo au mpenzi wako amkosea unategemea atakuelewa?

Kumbuka huyo ni mpenzi/mumeo hivyo ni lazima umheshimu na umtreat kwa upendo na sio kumfokeakadiri ya unavyojisikia hasa pale anapokosea. Kufoka kwa kunaweza kufanywa na mama mzazi lakini sio wewe mke.
Umeongea mulemule, sikutaka tu kumention point ya Unyenyekevu kwa makusudi kabisa. Nyinyi mnachotaka siku hizi sio mke mnyenyekevu, ila mke mnyonge.. Kila kitu "sawa mume wangu".

Umerudi usiku umechelewa siku ya kwanza ntakuuliza kulikoni, kwa sababu sio kawaida yako maybe unless ulisafiri kikazi. Ila ndo tabia yako kurudi usiku kila siku, kuna haja ya kukuuliza umetoka wapi?

Haya namwambia labda, bwana wewe hiki kitu A, B, C sio kizuri, sikipendi. Labda sipendi unavyorudi usiku umechelewa + umelewa sipendezwi na hiyo hali. Leo nikwambie kwa Unyenyekevu, kesho umerudia tena nakwambia kwa Unyenyekevu, na kesho kutwa umerudia tena nikwambie kwa Unyenyekevu Mmh? ?? Mwisho wa siku mtu anaona bora akae kimya, anakuignore tu. Ukiwahi sawa, ukichelewa sawa tu, utajijua coz wewe ni mtu mzima unajua unachofanya. Ndoa nyingi wanawake wameamua kukaa kimya kuwaignore, na ni kitu kibaya sana. Bora ukosee mtu hata akakukaripia, kuliko mtu anayekaa kimya akakuignore. Mtaenda wapi kwa maisha hayo? Ukosee afu mtu hata hakuulizi, mbona me ntakufa kwa kihoro khaa
 
Last edited:

Umemaliza kila kitu. Hope wamepata majibu
 
Umeongea vizuri yaani na uko sahihi kabisa,ila wakati mwingine sisi siyo vichaa tu kuanza kufoka foka hovyo ,kwa mtu anayejali hisia za mwenzake atamtaarifu mapema kwamba mke wangu mpenzi leo nitachelewa kuna moja mbili tatu,huyu mke akijakufoka atakuwa na yake mambo.

Pili mwingine unamtafuta na kutaka kujua Habari zake anakujibu labda yupo njiani anakuja unakuta toka saa 2 anakwambia anakuja kila ukimpigia ni yupo njiani tu mwisho mpka inafika saa 8 na mbaya zaidi hana tatizo lolote lililompata,kwanini hapa mke asikasirike maana unamdanganya kama mtoto.

Tatu mwingine anaaga vizuri kwamba yupo sehemu fulani lakini sasa ndo anajisahau kama vile yuko bachela, mtu anakuja full kalewa, maneno ya dharau n.k, Sawa piga starehe lakini jali basi na hisia za mwenzako kuwa na kiasi nenda na muda jua kuna mtu yupo anaumia juu yako.

Kwa kweli wanaume mngejua jinsi ambavyo huwa inatuumiza mnavyochelewa nyumbani msingesema,mtu unahaha unasema sijui Lipi limempata mwenzangu,usingizi unakata kabisa unasali sala zote ukiomba Mungu amlete mume salama, wengine hata chakula hali anamngoja mwenzake waje wale wote. SaSa kutokana na haya mahangaiko yote ya moyo aliyoyapata unakuta vile alivyodhani ndivyo sivyo unakuja mwingine kabisa anajikuta hawezi tena zuia hasira zake lazima akulipukie maana taswira nyingine inaumbika huyu katoka tu kwa mwanamke mwingine. Kikubwa ni mawasiliano tu yawepo na uwazi na ukweli tu, sisi siyo mbwa wa kufoka foka hovyo hata mbwa naye hufoka kwa sababu maalum.
 
Usemayo ni kweli kabisa mpendwa wangu na ninakubaliana na wewe 99.9%. Kuna wanaume wenye tabia hizo na wengi wao hufanya hivyo kwa sababu hawana upendo wa kweli kwa wenzi wao. Mtu mwenye upendo wa kweli siku zote huwa na huruma na kamwe hawezi kumfanyia mwenzake mabaya.
 
Kumbuka huyo ni mpenzi/mumeo hivyo ni lazima umheshimu na umtreat kwa upendo na sio kumfokeakadiri ya unavyojisikia hasa pale anapokosea. Kufoka kwa kunaweza kufanywa na mama mzazi lakini sio wewe mke.

Hata wanaume mnatakiwa kuwatreat hivyo wake zenu sio kuwafokea na wakati mwingine mnawapiga kabisa.
 
Umeongea mulemule, sikutaka tu kumention point ya Unyenyekevu kwa makusudi kabisa. Nyinyi mnachotaka siku hizi sio mke mnyenyekevu, ila mke mnyonge.. Kila kitu "sawa mume wangu".

Umerudi usiku umechelewa siku ya kwanza ntakuuliza kulikoni, kwa sababu sio kawaida yako maybe unless ulisafiri kikazi. Ila ndo tabia yako kurudi usiku kila siku, kuna haja ya kukuuliza umetoka wapi?

Haya namwambia labda, bwana wewe hiki kitu A, B, C sio kizuri, sikipendi. Labda sipendi unavyorudi usiku umechelewa + umelewa sipendezwi na hiyo hali. Leo nikwambie kwa Unyenyekevu, kesho umerudia tena nakwambia kwa Unyenyekevu, na kesho kutwa umerudia tena nikwambie kwa Unyenyekevu Mmh? ?? Mwisho wa siku mtu anaona bora akae kimya, anakuignore tu. Ukiwahi sawa, ukichelewa sawa tu, utajijua coz wewe ni mtu mzima unajua unachofanya. Ndoa nyingi wanawake wameamua kukaa kimya kuwaignore, na ni kitu kibaya sana. Bora ukosee mtu hata akakukaripia, kuliko mtu anayekaa kimya akakuignore. Mtaenda wapi kwa maisha hayo? Ukosee afu mtu hata hakuulizi, mbona me ntakufa kwa kihoro khaa

Embu naomba nikuulize hili swali, ukimfokea huyo mume/mpenzi wako ndo atakuelewa na kukusikia au ndo utazidisha matatizo zaidi na kumfanya asitake kukusikiliza?
 
nilichotaka kukuonyesha ni kuwa binadamu tuna ukomo wa kila kitu. Huo Unyenyekevu hautokuwepo kila siku, ipo siku mtu atachoka atakujibu tu na hata usivyotarajia. Kwa sababu hatupendi kuwafokea basi ndo isiwe sababu ya nyie kutunaaa nope. Kuishi na mtu afu anajitahidi kuignore as if haoni unachofanya si kitu chema honestly.
 
Back
Top Bottom