pole sana ndugu,
1. kati ya hao waliopunguzwa na wewe umo?
2. kama umo, ni kwamba watatakiwa wakulipe kwa kuvunja mkataba na wala haina kukwepa kwa sababu ni matatizo yao wao na sio yako, na pia sheria inaruhusu kuvunja mkataba kama shughuli ulizao kuwa unafanya ziimeisha au zimesitishwa au haziendelei tena
3. swala la jinsi ya kupunguza sio ishu sana, cha msingi ni wewe kulipwa kwa mkataba kuvunjwa kwa kuwa project haiendelei tena. au wakulipe stahili zako zote kwa hesabu ya miaka yote minne ya ajira yako kama wataweza.
Ukisoma Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 kwa pamoja na Kanuni za Utendaji Bora, 2007 utaona kuwa utamaduni wa zamani wa waajiri kuajiri na kufukuza, yaani, hire and fire unakatazwa na sheria na hivyo mwajiri, si tu anatakiwa kuwa na sababu za msingi za kumuachisha mwajiriwa kazi lakini pia sababu hizo ni lazima ziwe halali kisheria na ni lazima afuate utaratibu halali.
Katika mazingira uliyoyataja mwajiri anaweza kukuachisha kazi kutokana na mahitaji ya kiuendeshaji lakini kabla ya kufanya hivyo ni lazima afanye mashauriano na wafanyakazi ambao wanaweza kuathiriwa na zoezi hilo. Kama hajafanya mashauriano basi atakuwa amekiuka utaratibu halali.
Mwajiri anapoamua kumuachisha mwajiriwa kazi ni lazima amlipe malipo yafuatayo:-
- Mshahara wa kazi aliyoifanya kabla ya kuachishwa;
- Malipo ya likizo ya mwaka ambayo mwajiriwa hajachukua;
- Malipo ya likizo ya mwaka kwa mzunguko wa likizo ambao bado haujakamilika;
- Malipo ya notisi (mshahara wa mwezi mmoja);
- Malipo ya kazi iliyofanywa wakati wa muda wa ziada, sikukukuu na muda wa usiku (ambayo hayajalipwa).
- Kiinua mgongo; na
- Malipo ya usafiri hadi mahali alipochukuliwa wakati wa ajira.
Nashukuru kwa ushauri wako kaka Bandio. unapewa barua ya kuitwa kwenye kikao cha kujadili ili kuepuka kupunguza kazi na kisha hapo hapo mnafikia hatua ya kuambiwa kuwa tunakwenda kupunguza watu basi. na unapewa tarehe kuwa tarehe fulani tutataja majina ya watakao punguzwa na kupewa barua zao. kisha mnakwenda mtakuja kulipwa baada ya sisi kupata fedha kwa kuwa sasa atuna pesa na mkataba weneyewe ndio kwanza umetumikia mwaka mmoja na nusu. kweli inaingia akilini na niyeye aliyekupa huo mkataba na kukwambia kuwa nimekupa mkataba mrefu ili uendee ukakope bank, na yeye leo ndio mdhamini wa mkopo wangu bank. imekaaje hapo Bandio