Wandugu,
Mwanangu mmoja anataka kusomea nursing na shule kanieleza keshapata iitwayo MBAGALA NURSING SCHOOL. Nimeitafuta sana hii shule kwenye mtandao lakini sijaiona.
Nimewaandikia Tanzania Nurses and Midwives Council kutaka kujua kama hii shule imekuwa-registered na inatambuliwa na TNMC kabla sijatuma fees, lakini pia sijapata jibu.
Naomba kama yupo mtu yoyote anayejua chochote kuhusu hii shule anijulishe hapa ukumbini, kwani nasikia zipo shule tele za nursing ambazo ni illegal hapa nchini.