Naomba msaada wa Transcripts NACTE

WEKKI

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
477
Reaction score
146
Nilimaliza Chuo Mwaka 2020 Kada ya Afya. Mwaka 2022 Aprili Nikaomba maombi ya Transcript na Niliomba Niippokelee Mwanza ambapo ni Jirani.

Cha ajabu nikaambiwa kuwa Nitaikuta Mwanza. Nimeenda Ofisi ya Mwanza Wakaniambia kuwa haipo. Nikaenda Dodoma wakaniambia haipo. Nikaenda Ofisi za Dar Wakaniambia haipo ipo Mwanza. Nimerudi Mwanza Wakaniambia Haipo.

Hii ni zaidi ya Mwaka mzima nasubiri Watu wa Ofisi ya Mwanza wanipigie simu sijapata Msaada.

Je Kwanini NACTE wanaweka urasimu wa mtu kumpatia Cheti Cha transcripts. Kwanini Kama Cheti unapata Chuoni Kwanini vyeti visitumwe Chuoni.

Mpaka Sasa Sina msaada wowote na gharama za kutoka Mkoa kwenda Mkoa kufuatilia Transcripts imekuwa changamoto. Kama Kuna mtu ana msaada wa mawasiliano ya Moja Kwa moja anisaidie Ndugu zangu
 
Ebu fafanua vizuri wengine wageni Ina maana mitihani unafanya VETA MOROGORO cheti unachukua popotr unapootaka wewe siyo urudi chuon VETA MOROGORO au umekaaje ebu fafanua

NB
Hiyo VETA nimeweka mfano tu nataka kujua chuo gani ulisooma ukamaliza I mean jina la cho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…