Balvejmumt
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,149
- 2,784
Naomba niseme kitu hapa....Habari za usiku wapendwa Wana jf, jaman nasumbuliwa na allergy isiyoisha nimetokwa na vipele baadhi ya sehemu za mwili na vinawasha sana.Nimeenda hosp nikapimwa kweli nikakutwa na allergy ya baadhi ya vyakula vumbi nk,nimeacha kutumia vyote nilivoshauriwa lakini nikitumia dawa vinaisha alafu vinarudi tena naombeni ushauri this time nimetumia dawa lkn tatizo lipo palepale
Kama Kuna anaejua dawa za asili anisaidie please
Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Unaweza kukatazwa kula vyakula hata vyote kabisa lakini shida ikawa si vyakula ni kile unachoweka kwenye chakula au aina fulani ya dawa umezoea kutumia ndio zikawa zinakupa shida....
Mfano, kuna baadhi ya mafuta ya kupikia yamekuwa yakiwa sababishia watu allergy isiyo ya kawaida sijajua kuna tatizo gani huko ila tunaweza kuwaza je, mchezo wa uchakachuaji umeanza tena?
Nyingine ni matumizi ya aina fulani fulani za dawa mfano jamii ya dawa zenye sulphur kuna baadhi ya watu wanapata changamoto
Kwahiyo kwenye ishu ya allergy tafuta kile kinachounganisha na kusababisha allergy na siyo uangalie kimoja tu basi naamini kama ni hivyo kuna siku hata ukipika ugali utapata allergy sasa? Sorry
ITAFUTE SABABU USIKATE TAMAA