Badala ya kuhangaika kutibu, kama bado unaweza kudownload kutoka kwenye computer hiyo hiyo au nyingine yoyote, (Pia unaweza ku-download google Chrome kujaribisha kama utaweza kuingia mtandaoni bila kikwazo kilekile). Basi download Revo Uninstaller. Funga hizo browser zako zote, kisha tumia Revo kuziondoa zilizogoma. Tumia option ya mwisho ili kuondoa traces zote. Pia kwenye options za registry entries, select all kisha bonyeza delete.
Kama kuna bookmarks umetunza, unaweza ku-save kwenye folder pembeni kabla ya deletion ili kuzitumia utakapo re-install browsers zako. Hii inaonekana ni njia ndefu lakini kwangu mimi badala ya kupoteza muda naiona ya mkato maana unakuwa umetibu jumlajumla.