Habari za majukumu wakuu?
Nahitaji msaada wa information. Nimekuwa nikiishi nchi fulani ya Africa kwa miaka minne, sasa natarajia kurejea nyumbani( Tanzania). Nina gari langu amabalo nilikuwa nikilitumia kama miaka miwili hivi, nataka kurudi nalo home. Maana kuliuza kwa haraka sijapata mteja mzuri wa walau kurudisha hela yangu hata kiasi kidogo cha kuridhisha.
Nasikia kuna kamsamaha kidogo kwa Returning citizen, sema sijui mambo yanakuwaje, naomba kama kuna mkuu yeyote humu ndani anaweza kunisaidia information za uhakika.
Au kama labda naweza kupata mawasiliano ya mtu ambae anaweza kunisaidia kujua huo msamaha unakuwaje au labda kodi inakuwa ile ile ya kama gari lililoagizwa Japan?.
Natanguliza shukrani kwa msaada wanu.
Hiace Wagon, Ya 2001. Seat 9 passenger + 1 dereva, jumla ni viti 10.