Mimi ni mgeni kidogo katika masuala ya magari. Nimepata Gari kwa mtu anataka kuniuzia Carina SI. Naomba mwenye experience na Gari hii aniambie huwa yanatumia mafuta kwa kiasi gani kwa kilometer na ni mambo gani mengine ya msingi napaswa kuyajua before sijampa hela.
Mpe tu ela kaka ilo Kiwese c Tatizo kabisaaa chakuangalia body ipo poa? Na chini akuna shida Ile mikelele ya mashow cup ipo poa Na engine aitingishiki endapo kama Ivo vote vipoo poa mpatie tu ela yake Na kama kuna ubovu flani umkate kwenye pesa yake ila mukubaliane Mwisho Ni gari ambayo ukitaka kuitengeneza inatulia (inatengenezeka)
Usichukue SI maana ina cc1800 wakati carina Ti ina cc1500, si inatumia mafuta zaidi ya ti, mi ningekushauri uchukue ti maana ni sawa na si utofauti upo kwenye ukubwa wa injini