Naomba mnijibu pls

Tolowski

Senior Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
122
Reaction score
20
Nimekuwa nikijiuliza lakini nakosa jibu! Hivi ni kwa nini marekani kunaitwa unyamwezini? Au mmarekani anaitwa mnyamwezi? Sometimes mtu akiwa mjanja mjanja anaitwa mnyamwezi? Kuna uhusiano gani hapo?
 
Sema watumwa wa zamani wengi walitokea unyamwezini(Tabora) kutokana na nguvu zao wakafika marekani na asili yao unyamwezini sikonge..urambo etc
 
Wanaitwa wanyamwezi kwa kuwa wanyamwezi ni wajanja. Walifika katika miji mingi mapema kuliko makabila mengine ndio maana amekuwa mtani wa makabila mengi.
 
Kuna mtaa kule states unaitwa Nyamwezi str
 
wanaitwa wanyamwezi kwa vile wako magharibi. Mnyamwezi ni mtu kutoka magharibi.
 
Kwa kua weather ya us inafananana tabora, kwanza wanalima Kama taborao
 
Ni kwa sababu wamarekani wengi wana miili mikubwa na katika TZ hii wanyamwezi ndio wenye miili mikubwa kuliko makabila mengine!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…