Ndondwa
Member
- Jan 7, 2016
- 46
- 12
Nimeota kama nimechaguliwa kujiunga na chuo fulani hivi (kwa mazingira yake ni cha ufundi). Hcho chuo kina hosteli ambazo wanawake na wanaume hulala pamoja.
Siku tuliyofika kuripoti tulikuwa wanafunzi wengi wa kike na wakiume (siimfaham hata mmoja), tulipo ingia ifisini hatukumwona mwenyeji yeyote pale ndznie (hakuwepo mtu).
Baada ya hapo watu wakaanza kutembea tembea mule ndani ili kuyajua mazingira, mimi na baadhi ya watu tulizunguka kwa nyuma tukakuta kuna matunda mengi na nyani weusi wengi sana wakiwa na vitoto vyao(lakin hao nyani wala hawakutuogopa, wala kututisha, waliendelea kucheza juu ya miti na kula matunda.
Kwenye mlango uliofungwa kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wanataka kuufungua, baada ya kushindwa wakauvunja (walipo uvunja wala hawakuingia ndani, walicho kifanya wakaondoka maeneo yale).
Wakati huo mimi nlikuwa nimepanda juu ya mti (sikumbuki kuwa nlikuwa nakula matunda au la).
Chini ya mti niliokuwa nimepanda alikuwepo mdada ambaye kazi yake ilikuwa ni kuchuma matunda na kuwapiga nyani watoto (nyani hawakufanya chochote bali waliendelea kucheza na kula matunda), lakini baadae yule mdada alimpiga tawi moja jembamba ambalo mtoto mmoja wa nyani alikuwa amekaa, yule nyani alianguka chini.
Baada ya hapo, nyani wote wakanizonga mimi juu ya mti nlioupanda (hawakunishambulia wala kupiga kelele) walikuwa wakiniangalia tu huku wakisogea karibu yangu zaidi, mimi nlikuwa nikijitetea kwa kupiga kelele ya kwamba si mimi, huku ninyoosha kidole kuwaonesha yule dada alipiga mtoto wao.
Dada aliyekuwa chini ya mti alikuwa ametulia kimya kabisa (na hakufuatwa na nyani hata mmoja).
NDUGU WATALAAMU WA NDOTO NISAIDIENI TAFSIRI YA NDOTO HII. Nimeiiota ALFAJIRI.
Natanguliza shukurani