Nauli ni 15,000/= kwa zile basi zenye injini nyuma mfano Nani Kaona, Malewa, Lwangilo, Mbutta, nk. Ila ujiandae kushinda kutwa nzima kwenye hilo gari. Yaani unapanda saa 2 asubuhi, unafika Dodoma saa 10! Maana hizo chombo kila kituo zinasimama, na hazijawahi kuwa na haraka.
Ukipanda private pale Kihesa kwa Mzee Mgaya, utalipia pia 15,000/=, na utafika mapema Dodoma. (Wastani wa masaa 3 mpaka masaa 3 na nusu hivi.)
Kwa basi kubwa nzuri kama Shabiby, basi jiandae kulipa 18,000/=. Na ukipanda hilo basi, hutaingia kwenye 18 za wale Wamasai wa Migori na Izazi! Ambao kila kituo njia nzima utawakuta wanashuka/wanapanda.