Binafsi kama mwanamke kaniacha kwasababu anazozijua yeye nitaumia ila baada ya muda flani nitapona na nikishapona nakuwa sina tena upendo nae.
Nakumbuka niliwahi kuwa na msichana wangu wa kwanza ambae nilimpenda sana lakini alikuja kuniacha na kipindi hiko nilikua nasoma chuo ndo nimeingia mwaka wa pili.
Nilikuja kuonana nae baadae akiwa kadhoofika sana kiafya na akawa ananichangamkia kweli ila sikutaka kabisa kushiriki nae tendo la ngono, sio tu kwasababu niliona amedhoofika kiafya ila pia nilikua nishamtoa moyoni na sikua na mapenzi nae tena.
Mtoa mada sijajua umekaa muda gani mpaka kuanza kumtafuta tena huyo ex wako ila kama mwaka umepita na bado unamtafuta basi kuna haja ya wewe kujitathmini.